Leo jijini Mbeya, ndugu Oscar Kisanji (mwenye shati nyeupe pichani) mjumbe wa Halmashauri ya Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji, aliwasilisha na kuonyesha teknolojia ya zama hizo ambayo ilikuwa mali ya hayati Askofu Teofilo Kisanji- Askofu wa kwanza mzawa wa Kanisa la Moravian nchini Tanzania.
Ndugu Oscar alipiga sehemu ya santuri mbili kwa kutumia gramaphone- santuri moja ilikuwa sauti ya hayati Askofu akihubiri kwa lugha ya Kinyamwezi. Santuri ya pili ilikuwa kwa lugha ya Kinyakyusa na ilikuwa ya injili sehemu ya Matayo 25:1-13 inayohusu wanawali 10 na taa zao. Santuri hizi zilirekodiwa Uingereza mwaka 1957 alieleza ndugu Oscar Kisanji.
Aidha ndugu Oscar Kisanji alionyesha ngoma iliyokuwa ikitumika kuita watu kanisani wakati wa Askofu Kisanji. Familia ya Kisanji imekabidhi vifaa hivi-ngoma na gramaphone- kwa TEKU ili vihifadhiwe kama kumbukumbu ya Chuo Kikuu kilichobeba jina la hayati Askofu Teofilo Kisanji.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...