Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dk Terezya Huvisa akitoa amri ya Kuifungia Hoteli ya Giraffe Ocen View iliopo Jijini Dar es Salaam wakati wa Ziara ya Kutembelea Hoteli zilizopo pembezoni mwa fukwe ya Bahari ya Hindi, jijini Dar es Salaam.

Lulu Mussa na Ali Meja - Ofisi ya Makamu wa Rais

Waziri wa Nchi wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira Dk. Terezya Huvisa hii leo ameendelea na ziara ya kikazi ya kukagua hali ya mazingira katika hoteli zilizopo pembezoni mwa fuke za bahari ya hindi, jijini Dar es Salaam.

Ziara ya leo imeanzia katika hotel ya Giraffe Ocean View, na katika hali ya kushangaza maagizo aliyotoa Naibu Waziri Charles Kitwanga katika hoteli hiyo mapema mwezi huu ya kurekebisha mfumo wa majitaka na kuweka fukwe katika hali ya usafi hayajazingatiwa.

Hatua kali zimechukuwa wa Hotel hiyo ikiwa ni pamoja na kufungiwa mpaka hapo itakapotimiza masharti yaliyowekwa kwa mujibu wa sheria ya mazingira ya mwaka 2004. “Naifunga Hotel hii ya Girafee mpaka hapo itakapotimiza masharti ya hifadhi ya mazingira” alilisitiza Dkt. Huvisa.

Sambamba na hilo Waziri Huvisa ameipongeza Hotel ya Beach Comber kwa kuwa na mkakati endelevu wa mfumo wa maji taka na hifadhi ya fukwe kwa ujumla. Dkt. Huvisa amesema kuwa zoezi hilo ni mkakati endelevu wa kukagua hoteli zote na viwanda, Ofisi ya Makamu wa Rais – Idara ya Mazingira kwa kushirikiana na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) wanafanya kazi hiyo kwa kikamilifu.

Kwa mujibu wa sheria ya Mazingira ya mwaka 2004, Hoteli na Viwanda vyote vilivyoanzishwa kabla ya matumizi ya sheria hiyo vinatakiwa kufanya (Environmental Audit) na baada ya sheria ya Mazingira hutakiwa kufanya Tathmini ya Athari za Mazingira (Environmental Impact Assessment).

Katika ziara ya siku mbili iliyofanywa na Waziri Huvisa pamoja na Naibu wake Charles Kitwanga imepelekea kuchukua hatua kali za kisheria ambapo Hotel ya Double Tree na Giraffe Ocean View zimefungiwa mpaka hapo zitakotimiza masharti waliyopewa.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dk Terezya Huvisa akitoa Maelekezo kwa Meneja wa Hoteli ya Girafee Ocen View wakati wa ziara ya kutembelea Hoteli zilizopo kwenye fukwe za Bahari.
Hoteli ya Girafee Ocen View iliofungiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Terezya Huvisa wakati alipotembelea leo katika mfululizo wa ziara ya kukagua hali ya Mazingira kwenye fukwe za Bahari.
Uchafu katika Ufukwe wa Hoteli ya Girafee Ocen View.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa


  1. Dr Huvisa ni ngangari, lakini kwa kweli kazi ya kukagua na kuzifunga hizi hoteli ingefanywa na wakaguzi wa hoteli, na waziri aendelee na kazi nyingine nzito.

    ReplyDelete
  2. Duuh! Ili mradi isiwe ni kwa sababu za kisiasa, ila kama ni kwa majukumu big up, ila mlikuwa wapi sikuzote hizo?

    ReplyDelete
  3. Anonymous wa kwanza,Thu Dec 20, 05:48:00 PM 2012
    Nakuunga mkono. Nilisema hivyo kwenye maoni ya awali, Waziri alipoiifungia Double Tree. Najua ni Hotel kubwa, lakini mpaka Waziri aje? Wafanyakazi wake wako wapi? Manaibu Waziri, n.k Kama yeye mwenyewe Waziri ameamua kuiingia kazini moja kwa moja, basi nimeipinda hii tabia-Endelea hivyo vivyo labda tutakuwa na Rais Mwanamke 2015, ndiyo mabadiliko ya kweli.

    ReplyDelete
  4. hili haliwezi kuwa zoezi endelevu kwa sababu waziri hana muda wala uwezo wa kukaguwan kila hoteli nchi nzima. Ilitakiwa aanze na watendaji wizarani kwake, ikiwa kawashindwa watumishi wa chini yake basi bila shaka hili ni joto maji ya moto hayaunguzi nyumba

    ReplyDelete
  5. Chochote kinachofanyika ni lawama tu. Lawama imejengeka, imekuwa tabia, hulka, kazi na hobby. Bigup Mr and Mrs Lawama anons! Loh

    ReplyDelete
  6. Anonymous wa tatu: Thu Dec 20, 08:09:00 PM 2012, umelonga pointi

    ReplyDelete
  7. Wasaidizi wake waligonga mwamba.Maagizo yao hayakufanyiwa kazi,ikabidi Waziri Mwenyewe aingie kazini.

    ReplyDelete
  8. Tanzania mambo huwa ya moto mwanzoni lakini hupoa bila taarifa.....hapa ni kwa sabb hajaguswa kigogo mwenye hotel. Akiguswa tu mtasikia huyu mama hana kazi

    ReplyDelete
  9. Kwa hilo nampongeza Waziri ingawa ni jukumu la Baraza la Taifa la mazingira. Namuomba Waziri ( ni Waziri sababu watendaji wake wameshindwa kazi ) aende Mbagala kuona jinsi wananchi wanavyopata taabu ya moshi unaotoka viwandani wakati wa jioni ( Viwanda vya Nondo na Kiberiti nk. Nadhani baada ya miezi mitatu kuanzia sasa madhara makubwa ya kiafya yatatokea.

    ReplyDelete
  10. Nyinyi hamuoni Mwakyembe na Pombe wanafunika. Mwajua siri ya urembo basi kila waziri lazima ajaribu angalau kuwafikia hao

    ReplyDelete
  11. Mama waziri umetaim muda mbaya wa X-MAS na NEW YEAR?....

    ReplyDelete
  12. serikali za mitaa inatakiwa iwe na uwezo wa kufunga hizo hotel.kwai mpaka waziri jamani?au ndo mapatoz ya serikali kuu kwani mitaa wanapatia wapi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...