Wazalendo,
Napanda kuchukua nafasi hii kuwafahamisha kuwa kutokana na maombi ya
wanataaluma wengi kuwa mwishoni mwa mwezi desemba wanakuwa likizo.
Hivyo basi TPN imesikiliza maoni hayo na tumeamua kuisogeza mbele siku hii 
ya wanataaluma Tanzania hadi mapema mwaka 2013. 

Siku na Mahali tutawajulisha hapo baadae, mambo yote yaliyopangwa
yatafanyika. 
Kutokana na kusogezwa mbele nachukua fursa hii kuwafahamisha kuwa bado 
tunapokea maombi ya wanaotaka kutunikiwa tuzo; unaweza ukampendekeza mtu au 
ukajipendekeza mwenyewe , ambatanisha CV na ueleze ni kwa nini upewe au 
unayempendekeza apewe tuzo husika (soma email ya chin kwa maelezo zaidi).

Naomba tuendelee kushirikiana na kupeana ushauri kufanikisha siku hii. 
Nawashukuru wote waliojitokeza kudhamini tukio hili na pia walijitokeza
kuchangia mawazo kufanikisha siku hii. Makampuni yaliyojitokeza kudhamini ni pamopja na ya umma na binafsi. 
Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaosababishwa na kuahirishwa kwa tukio 
hili ,naomba tuendelee kushirikiana.

Nawatakia wote kila heri ya kipindi hiki cha siku kuu za Krismasi,
mapumziko na Mwaka mpya mwema 2013. 
Wanataaluma tuna nafasi ya kutumia taaluma zetu kuleta mabadiliko chanya kwa
faida ya Taifa letu.

Mungu awabariki wote, 
Mungu ibariki Tanzania.

Phares Magesa
Rais- TPN

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...