Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama akimkabidhi sehemu ya msaada wa vyakula Mkurugenzi wa Kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Mwandaliwa, Halima Ramadhani. Mbali ya kukabidhi vyakula hivyo, Msama pia alikabidhi hundi ya sh milioni 1.5 kwa ajili ya kulipia ada za wanafunzi waliofukuzwa shule. Msaada huo umetokana na mapato ya tamasha la Pasaka, hafla hiyo ilifanyika Mbweni nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama akikabidhi sehemu ya msaada wa vyakula
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama akikabidhi sehemu ya msaada wa vyakula
Mkurugenzi
wa kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama akimkabidhi hundi ya sh.
milioni 1.5 Mkurugenzi wa Kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika
mazingira magumu cha Mwandaliwa, Halima Ramadhani kwa ajili ya kulipia
ada za wanafunzi waliofukuzwa shule. Mbali ya kukabidhi hundi, Msama
alikabidhi msaada wa vyakula mbalimbali vikiwa na thamani ya sh milioni 3
zilizotokana na mapato ya tamasha la Pasaka, hafla hiyo ilifanyika
Mbweni nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.
Dua ya kumshukuru mungu ikisomwa.Picha zaidi Bofya hapa
jamani hata kama ni kutoa msaada tuheshimu dini za wenzetu, huwa wakiwa wanaswali wanavuaga viatu. sasa mwenzetu kwa vile umepeleka msaada umeona kuvua viatu haikuhu siyo vizuri hata kidogo na mbaya zaidi umevikanyaga. na ingependeza zaidi kama usingeweka mikono yako katika hali ya uvivu namna hiyo hapo watu wanasali na kumheshimu Mungu. mimi ni mkristo saafi sijafurahishwa na tabia yako. kingine sioni umuhimu mtu akienda kutoa msaada anaita wapiga picha waandishi wa habari ili atolewe magazetini kwenye blogs nk. jamani hiyo ni sadaka hamna haja ya kutangazia ulimwengu. Mungu anaona mtapata thawabu zenu tu lakini kwa mtindo huu mh. michuzi naomba mnooo usibane meseji hii. wewe ni mwadishi unajua maana ya freedom of speech! HAPPY NEW YEAR!
ReplyDeleteNi kweli wee anon umesema hapo juu, hivyo viatu, na hiyo mikono, haoni wenzake walivyoweka mikono vizuri, sasa jamani tunatoa missada, ili tupate baraka, swawabu kwa mumba, tujalibu kujinyenyekeza basi, mungu anatuanglia mioyo yetu, na matendo yetu, weka mikono vizuri upate baraka,swawabu, hata mimi mkristo, lakini tukija kwa upande wa imani lazima tueshimu, na matendo yetu yawe ya kupendeza, machoni pa wanadamu na mumba
ReplyDeleteWewe anon wa kwanza sikubaliani nawe. Hata kama kakosea kidogo lakini anachofanya ni kizuri na inabidi apongezwe. Ni heri yeye aliyefanya jambo jema kwa 70% na kukosea kwa 30% kuliko wewe usiyefanya chochote!!
ReplyDeleteKuhusu kutangaza kutoa misaada nadhani ni vizuri sababu inahamasisha wengine. Yeye ni mfanya biashara hasa wa nyimbo za injili na mimi kama munuzi napoona anatoa misaada na kutaja kiwango napata moyo kwamba naponunua bidhaa zake vile vile nasaidia wengine. Kutangaza au kutotangaza misaada ni uamuzi wa mtu na hii si issue. Hata huko nje mlipo watu wengi tu wenye uwezo wanatangaza wanapotoa misaada.
we mdau wa kwanza acha mawivuz wewe, jamaa ametoa msaada, waliosaidiwa roho zao nyepe, apigwe picha au la yote ni sawa tu. kwanza picha zinasaidia kuwaelimisha watu wawe na nyoyo za kujitolea, give constructive critcism na siyo longolongo tu!, what went well? what did not go well? and what should be done to make things better in the future.
ReplyDeletemimi nataka kuliza hivi asiye dini nyingi kwa nini anatoa msaada kwa siiyo dini yake? hivi anataka nini? au anapata nini? agenda ya siri ipi? halafu kwa nini usimheshimu mwenzako katika dini yake, unajua watu wanatoa viatu na kuweka mikono vizuri kama hutaki kujihusisha na sala yao basi kwanini uwe upo
ReplyDeletenatumia wadau wenzangu watanijibu
Basi mkaushie !!!
ReplyDeleteHalafu hajamuona padiri akiweka mikono yake akiomba hamna tafauti na waislamu. Mungu ni mmoja tu anavyoombwa kwa vitendo hamna tafauti wote tunapiga magoti. Ila kwa dua hii hana haja ya kuvua viatu akipenda.
ReplyDelete