Pichani kulia ni Mkurugenzi wa Prime Time Promotions Ltd,Joseph Kusaga akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi millioni 105 kwa uongozi wa timu ya Yanga kwa ajili ya maandalizi ya mkutano wao mkuu pamoja na mechi ya kirafiki ya kimataifa katika kukamilisha shamrashamra za kusindikiza mkutano huo wa kwanza wa uwazi wa kihistoria kwa Club ya Yanga. 
Mkurugenzi wa Prime Time Promotions Ltd,Joseph Kusaga na Makamu Mwenyekiti wa Club ya Yanga,Clement Sanga wakikabidhiana mikataba yao ya makubaliano ya kikazi.
 Mkurugenzi wa Prime Time Promotions Ltd,Joseph Kusaga akitiliana saini ya makubaliano na club ya Yanga kuhusiana na makubaliano ya timu ya Yanga  kusaini mkataba wa maelewano na kampuni ya Primetime Promotions Ltd,ambapo Prime Time Promotions imekubali majukumu ya matayarisho yote ya mkutano wa wanachama wote wa Yanga uliopangwa kufanyika Januari 19 2013.
Mkurugenzi wa Prime Time Promotions Ltd,Joseph Kusaga akifurahia jambo na baadhi ya Wanahabari mara baada ya kutiliana saini mikataba yao ya kikazi na Club ya Yanga,uliofanyika mapema leo kwenye makao makuu ya ofisi za club hiyo,Jangwani jijiini Dar
Mkurugenzi wa Prime Time Promotions Ltd,Joseph Kusaga akizungumza machache kuhusiana na makubaliano yao ya kikazi na Club ya Yanga ikiwemo sambamba na makabidhiano ya mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 105 yaliyotolewa na kampuni ya Prime Time Promotions Ltd.
Pichani kati ni Makamu Mwenyekiti wa Club ya Yanga,Clement Sanga akizungumza mapema leo kwenye makao makuu ya timu hiyo na Waandishi wa habari kuhusiana na timu ya Yanga  kusaini mkataba wa maelewano na kampuni ya Primetime Promotions Lt,ambapo Prime Time Promotions imekubali majukumu ya matayarisho yote ya mkutano wa wanachama wote wa Yanga uliopangwa kufanyika Januari 19 2013.Kushoto ni katibu mkuu wa Yanga Lawrence Mwalusako na kulia ni Mkurugenzi wa Prime Time Promotions Ltd,Joseph Kusaga.

Aidha katika mkutano huo imeelezwa kuwa matayarisho hayo yatahusisha ukumbi na viambatanisho vyote muhimu,ikiwemo Live TV coverage na matangazo mbalimbali ya kuhamasisha mafanikio ya mkutano.


Aidha katika kuongeza mapato kwa maendeleo ya club na matayarisho ya kumalizia ligi, Prime Time Promotions Ltd,imetoa milioni 105 mapato ya uhakika kwa timu ya Yanga na Prime Time Promotions  itaandaa mechi ya kirafiki ya kimataifa katika kukamilisha shamrashamra za kusindikiza mkutano huo wa kwanza wa uwazi wa kihistoria kwa Club ya Yanga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Hivi muheshimiwa umekosa sehemu ya kusaidia hayo mahela yote!!??au unalako jambo?maana binafsi sijaona maantiki hapo.Vilabu vikubwa kama hivyo inawezekanaje kushindwa kugharimia mikutano yao??

    ReplyDelete
  2. Hiyo Cheque imeandikwa One Hundred Million and five ambayo sawa na 1,000,005.
    Au ndo wengine tumefeli BAM form 6

    ReplyDelete
  3. Huo ni msaada au ushirikiano wa kibiashara?hongereni kwa ubunifu,maana najua hao jamaa hawana free lunch,always kwao ni nipe ni kupe,ila kwa wanachama wetu watakuwa wanacheza ngoma bila hata kujua undani wake....itafahamika tu

    ReplyDelete
  4. Yanga s.c. NA Simba s.c !

    Mkumbuke ya kuwa bure ghali !!!

    ReplyDelete
  5. We better leave MEN AT WORK!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...