Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akitoa maamuzi makali yaliyopelekea kuteua Kamati ya kusimamia kumaliza mgogoro wa maeneo ya kilimo katika vijiji vya Dole, Ngurueni na Ndunduke Dole mara baada ya kupokea kero za Wakulima hao.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akishuhudia nyaraka bandia walizopewa baadhi ya watu walio nje kabisa ya maeneo ya kilimo ambapo Mkurugenzi wa Ardhi Nd. January Fusi alizibaini baada ya kuwasilishwa kopi zake na wakulima hao. Kati kati ya Balozi Seif na Ndugu January Fusi ni Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo na Mali Asili Zanzibar Nd. Alfan Othman aliyevaa kofia ya kiua.
Mwenyekiti wa kufuatilia matatizo ya wakulima wa Dole na Ngurueni Bwana Daudi Sirus Mukaka akiwasilisha maazimio yao mbele ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif ambayo walikubaliana katika vikao vya awali lakini hayajatekelezwa na hatiame kuleta kero.
Baadhi ya Wakulima wa Dole, Ndunduke, na Ngurueni Wilaya ya Magharibi wakiwa katika kikao cha kuwasilisha malalamiko yao ya kucheleweshewa kupewa umiliki wa maeneo ya kilimo mbele ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hayupo pichani hapo skuli ya Wazazi Dole.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Wandugu zetu Visiwani:

    Ya nini yote mkafarakana kugombea ardhi vijijini huko Dole, Ndunduke na Ngurueni Wilaya ya Magharibi-Zanzibar ilhali mkiwa katika Muungano mnayo nafasi ya kuja kulima Kilosa, Magu,Ludewa na Kwimba (Bara) ndani ya JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA!

    SISI BARA NA NINYI VISIWANI NI NDUGU, MTAKAPOFIKA MTAFUATA TARATIBU HIZI:

    1-MTATOA TAARIFA KWENYE MABARAZA NA SERIKALI ZA VIJIJI MTAKAZOFIKIA.

    2-MTAJITAMBULISHA KWENYE KAMATI ZA USALAMA HUKU MKITOA VIELELEZO VYA MLIKOTOKA ILI KUHAKIKIWA.

    3-MTASAJILIWA KAMA WANAVIJIJI WAPYA.

    4-MTAPANGIWA MAENEO YA ARDHI KWA KUPEWA MASHAMBA YA KILIMO.

    5-MTASHIRIKISHWA KAMA WANANCHI HALALI KTK KILA HATUA YA UONGOZI WA UMMA KUANZIA NGAZI ZA VIJIJI.

    MNAONA SASA HII FAIDA NA UMUHIMU WA MUUNGANO?

    ReplyDelete
  2. Assalam Alaykum!

    Ni vizuri tukakumbushana.

    Zanzibari huko mu Waislamu wazuri, hivyo sio busara kufarikiana kwa ajili ya vitu vya kiduniya.

    Mkumbuke kila kilicho mbele yetu ni cha kupita huku Dunia ikiwa ni makazi ya muda na hivyo kila kitu tutakiacha hapahapa duniani!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...