Mbunge wa Jimbo la Ukonga,Mh. Eugean Mwaiposa (katikati) akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Dar es Salaam mapema leo asubuhi wakati wa kutangaza uzinduzi wa Mkakati wake wa kuwainua kiuchumi wananchi wa Jimbo lake la Ukonga kupitia Mradi aliouanzisha ujulikanao kama "JAMII NA MAENDELEO UKONGA",ambapo amefanikiwa kuvikusanya vikundi vya wafanyabiashara ndogo ndogo waliopo kwenye Jimbo la Ukonga na kwa umoja huo pia ameanzisha Saccos ya Jimbo itakayowawezesha wafanyabiashara hao kupata mikopo ya kuendeleza biashara zao inayotambulika kwa jila la UKONGA VICOBA SACCOS LTD (UVICOSA).Wengine pichani ni Mwenyekiti wa Muda wa Saccos hiyo,Bi. Adivela Ruge (kulia) na Katibu wake,Bi. Mary Katobes.
 Katibu wa Ukonga Vicoba Sacos (UVICOSA),Bi. Mary Katobes (kushoto) akiongea wakati wa kuwahamasisha wananchi wa jimbo la Ukonga (kupitia vyombo vya habari) kujitokeza kwa wingi kujiunga na Sacos yao hiyo.
Meneja wa Mradi wa Jamii na Maendeleo Ukonga,Suzan Miseda akiongea katika mkutano huo na Waandishi wa Habari.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Hongera Mh. Mama Mwaiposa, kwa kuonyesha njia Ukonga, hayo ndiyo mambo....

    ReplyDelete
  2. Hongera Mh. Mwaiposa na timu yako na Mungu akusaidie uikamilishe kazi kwa maendeleo ya jimbo.

    ReplyDelete
  3. Hongera Mh. Mama Mwaiposa, umeonyesha njia, Mungu atakusaidia uimalize kazi, maendeleo hayadondoki kama mvua, yanaletwa na watu!!

    ReplyDelete
  4. Mheshimiwa mbunge huu ni mwendelezo wa kukabiliana na changamoto za maendeleo ndani ya jimbo la Ukonga.
    Kila kata ndani ya jimbo la Ukonga inakabiliwa na changamoto katika sekta za elimu,afya,miundombinu ya nishati ya umeme,usafirishaji wa abiria na ujasiria mali.Kutokana na ongezeko la watu katika mtaa wa Kitunda Mzinga umeibuka uhitaji wa kusogeza huduma za kijamii karibu za idi na watu ili kuwapunguzia adha ya kupanda mlima na kuzifuata eneo la Kitunda (Shule)kati.Huduma ya usafirishaji wa abiria ni changamoto nyingine kutokana na barabara zilizopo kutokidhi viwango vya kupata ruti ya Posta na Kariakoo na kuwapa wananchi ugumu wa maisha kwa kuendelea kulipa nauli ya Sh.500.00 kwenye Kibeberu,Mwanagati,Nyantira na Sh,1000.00 kwa wale wa Magole ukitokea stendi yenye tope na kero nyingi pale Banana.Mahitaji ya wakazi wengi ni busara za mamlaka husika kujitahidi kuwaunganisha na Mbagala Rangi Tatu kupitia Magole na Temeke Tandika kupitia Mwanagati.Kwa ujumla huenda likawa jambo jema sana iwapo Mzinga itaingia kwenye orodha ya kata mpya za Manispaa ya Ilala.

    ReplyDelete
  5. Ujenzi wa kivuko katika eneo la mnara wa Vodacom mwanagati kwenda Buza manispaa ya Temeke ni kichocheo kikubwa cha maendeleo ili wananchi wa manispaa za Ilala na Temeke waweze kuwasiliana na uwepo wa uhakika wa usafirishaji abiria kwa njia ya barabara kati ya Kitunda ,Tandika na kwenda katikati ya Jiji .


    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...