Mtangazaji Mwandamizi wa Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Ujerumani (Deutsche Welle), Josephat Charo (kulia) leo hii amekabidhiwa rasmi mikoba ya kuwa Mhariri Mwandamizi wa Idhaa hiyo,iliyoachwa na Othman Miraji aliyestaafu hivi karibuni. Kushoto ni Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili,Andrea Schmidt mara baada ya kutangaza wadhfa huo katika hafla maalum iliyofanyika mjini Bonn,Ujerumani.
Pichani toka kushoto ni Mhariri Mwandamizi wa Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Ujerumani (Deutsche Welle),Josephat Charo, Abdul Mtullya, Sylivia Mwehozi na Bruce Amani wakati wa hafla maalu,iliyofanyika leo mjini Bonn,Ujerumani.
Kutoka kushoto ni Josephat Charo, Nina Markgraf na Sudi Mnette wakiwa pamoja kwenye hafla hiyo.
Mdau Sudi Mnette akiwa na zawadi ya chrismas na mwaka mpya ya kitabu ambacho alipewa kila mfanyakazi wa Dw na Mkuu wa Idhaa Andrea Schmidt.
wafanyakazi Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Ujerumani (Deutsche Welle) wakifurahi pamoja baada mkuu wa Idhaa hiyo Andrea Schmidt kumtangaza Josephat Charo kuwa ni miongoni mwa wasaidizi wake wa karibu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Hiiii!!!! manitu ! Sudi Mnette hiyo zawadi ya kitabu ni nzuri sana,maana vijana wa uswahili shule ni sawa na kituo cha Polisi

    ReplyDelete
  2. Duh! hii ya leo inanidhamu kweli Sudi kashindwa kupiga Konozi kwa Mjerumani Nina ,si unajua wazungu nidhamu kazini,ingekua wamatumbi watupu we acha si konozzzzzz!!!!! hizo

    ReplyDelete
  3. Mbona Nina kapiga nusu-konoz.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...