Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mh, Angellah Kairuki akihutubia katika maadhimisho ya siku ya msaada wa kisheria Tanzania inayoadhimishwa leo tarehe 8/12/12 katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar Es Salaam. Wananchi mbalimbali watapata msaada bure kutoka kwa wanasheria wa hapa nchini. Kauli mbiu ya siku hii ni 'Msaada wa kisheria ni haki ya Binadamu na ya Kikatiba.
Bi. Fortunata Kitokesya wakili kutoka chuo kikuu cha Dar Es Salaam akimshukuru Mh. Kairuki baada ya Hotuba yake katika siku ya msaada wa kisheria viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar Es Salaam leo.
Baadhi ya Wananchi na Mawakili waliohudhuria maadhimisho ya siku ya msaada wa kisheria Tanzania wakimsikiliza mgeni rasmi katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar Es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...