Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli,Mh. Edward Lowassa na mkewe Mama Regina Lowassa wakiungana na Wakristo wengine kwenye ibada ya Sikukuu ya Krismas iliyofanyika leo kwenye Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),Mwanakwerekwe Zanzibar.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli,Mh. Edward Lowassa akitoa salaam za Xmas kwenye Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),Mwanakwerekwe Zanzibar mara baada ya ibada ya Sikukuu hiyo leo.Mh. Lowassa yuko visiwani humo kwa mapumziko ya sikukuu hiyo,ambapo amewataka watanzania kusherehekea sikukuu hizi za krismas na mwaka mpya kwa amani na upendo huku tukilinda umoja na mshikamano uliojengwa na waasisi wetu Mwalimu Julius Nyerere na Sheikh Abeid Karume.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...