Mshambuliaji wa timu ya Mikocheni United Keneth Mutta (kulia) akichuana na Jerry Santo wa Mikocheni City katika mechi ya fainali ya kombe la Diwani iliyofanyika kwenye uwanja wa shule ya Msingi Ushindi, Mikocheni, Dar es Salaam jana. City waliibuka mabingwa kwa mikwaju ya penati 4-3.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni na Diwani wa Kata ya Mikocheni, Yusuf Mwenda akikabidhi kombe la Diwani kwa Nahodha wa timu ya Mikocheni City, Abdul Abdallah baada ya kuibuka mabingwa wa kombe hilo kwa penalti 4-3 katika mechi ya fainali dhidi ya Mikocheni United iliyofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Ushindi, Dar es Salaam jana.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni na Diwani wa Kata ya Mikocheni, Yusuf Mwenda (mwenye fulaa ya mistari) akikabidhi pikipiki yenye thamani ya shilingi milioni 1.7 kwa Nahodha wa timu ya Mikocheni City, Abdul Abdallah baada ya kuibuka mabingwa wa kombe hilo kwa penalti 4-3 katika mechi ya fainali dhidi ya Mikocheni United iliyofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Ushindi, Dar es Salaam jana.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...