Pichani kulia ni Mkurugenzi wa Clouds Media Group,Joseph Kusaga akiwakaribisha wageni wake,akiwemo mwanamuziki nyota wa dansi ndani ya kundi la Wenge BCBG,kutoka nchini DRC-Congo,JB Mpiana (pichani kati) kwenye hafla fupi ya chakula cha usiku iliyofanyika kwenye kiota cha maraha cha Escape 2,kilichopo Kunduchi jijini Dar,hafla hiyo pia ni sehemu ya muendelezo wa shamra shamra za maadhimisho ya miaka 13 ya Clouds FM tangu kuanzishwa kwake hapa nchini.
Mkurugenzi wa Clouds Media Group,Joseph Kusaga akiwakaribisha wageni wake na kuzungumza nao machache na kuhakikisha wanapatiwa chochote kitu.
Mkurugenzi wa Clouds Media Group,Joseph Kusaga akimtambulisha mke wake Johayna Kusaga (ambaye ndiye Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Prime Time Promotions Ltd) kwa Mwanamuzik JB Mpiana na kwa wageni wengine waliofika kwenye hafla hiyo ya chakula cha pamoja.
Mkurugenzi wa Clouds Media Group,Joseph Kusaga akimkaribisha mgeni wake JB Mpiana kwenye chakula
Pichani ni baadhi ya Washiriki wa shindano la Miss East Afrika 2012 ambao pia walialikwa kwenye chakula cha pamoja ndani ya kiota cha maraha cha Escape 2,kilichopo Kunduchi jijini dar.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...