Na Abdulaziz,Lindi

UPEPO mkali uliombatana na mvua kubwa umeziathiri baadhi ya nyumba huku shule ya sekondari ya Mnacho wilayani Ruangwa ikipata athari kwa kiasi kikubwa baada ya madarasa sita kuezuliwa mabati na baadhi ya wanakijiji kupata majeraha na kusababisha wakazi wengine kukosa mahali pa kuishi.

Upepo huo uliotokea jana ni mfufulizo wa matukio hayo kwa vijiji vya kata hiyo ambapo awali mwanzoni mwa mwaka huu uliezua madarasa mawili ya shule hiyo.

Akitoa taarifa ya maafa hayo ya jana katika kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Ruangwa leo, Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo,Bw Reubern Mfune alieleza kuwa Kufuatia kuwepo kwa tukio hilo lilitokea jana jioni Ofisi yake ilifika eneo la tukio akiwemo na mkuu wa wa Mkoa wa Lindi,Ludovick Mwananzira na tayari wamepelekwa wataalamu kutathimini athari hizo ili shule hiyo inayotarajiwa kuanza muhula jan 14 Halmashauri yake itashirikiana na ofisi ya mkuu wa wilaya kuhakikisha hali ya shule inakamilishwa.

Aidha Mkurugenzi alibainisha katika kikao hicho cha baraza la madiwani kuwa Katika maafa hayo ambayo kwa kiasi kikubwa yaliathiri shule hiyo bado ni changamoto katika Halmashauri yake kufuatia kupangawa kupokea wanafunzi 92 wa kidato cha kwanza na inatarajiwa kufunguliwa jan 14,2013 Katika maafa hayo Mtu mmoja alijeruhiwa na kukimbizwa hospitalini

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Nikiangalia hapo naona kabisa kwamba Mhandisi aliyekubali hayo majengo mikono yake imejaa damu za walioumia na aliyekufa. Kenchi hazikuwekewa hata waya zililazwa juu ya ukuta tu. Lakini kwa sababu ya rushwa wanahatarisha maisha ya watoto wetu tu kwa sababu wao wanasoma International schools.

    ReplyDelete
  2. ni kweli kabisa,au basiwangeweka mbao nene.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...