Baada ya kila mmoja kupewa vyombo vipya na Konyagi, bendi pizani za Msondo Ngoma na Mlimani Park Orchestra (Wana Sikinde Ngoma ya Ukae) zitapambana siku ya Krismasi katika ukumbi wa Equator Grill, Temeke.
Mpambano huo umeandaliwa na kampuni za Bob Entertainment na Keen Arts na kudhaminiwa na kinywaji cha Konyagi.
Mratibu wa mchuano huo Joseph Kapinga amesema pambano hilo litakuwa la kusherekea sikukuu ya Krismasi na kufunga mwaka 2012.
Kapinga alisema kuwa pia pambano hilo litaamua ni bendi gani bora kati ya magwiji hao wawili wa muziki wa dansi nchini kwa mwaka 2012.
Mratibu huyo alisema bendi hizo zitapiga jukuwaa moja lakini kila moja atatumia vyombo vyake ili kuondoa malamiko ya kuhujumiwa. Kila bendi itatumia muda wa saa moja kabla ya nyingine kupanda jukwani.
“Litakuwa pambano la aina yake ukizingatia kuwa hii itakuwa ni mara ya pili kwa bendi hizo kupambana siku ya Krismasi tangu zianzishwe. Mwaka jana zilipambana katika TCC Club Chang’ombe,” alisema Kapinga.
Alisema mchuano huo itaanza saa tisa mchana hadi liamba.
Kwanza niwapongeze Konyagi kwa dhati kabisa,kwa kitendo cha kizalendo na kishujaa na pia ubunifu wa hali ya juu kabisa wa kibiashara,kuwapa nguvu (support)bendi zetu mbili Kongwe hapa nchini,Sikinde na Msondo,kwa kuwapatia Vyombo au Ala mpya za Muziki wa Dansi!Hongera sana,kwa Uongozi mzima wa kampuni ya Konyagi.Sio kitu kidogo.Wengine walishindwa,lakini wao Wameweza.Sisi Wateja wenu tutakuwa nanyi bega kwa bega.Kwa upande mwingine,wao wenyewe wana bendi wa hizo bendi mbili,kufanikiwa kwao kutatokana na hakika kutategemea zaidi Juhudi zao Binafsi,juhudi binafsi na ubunifu wa kila mwanabendi au mwanamuziki,lakini pia,juhudi za kikundi kizima kwa pamoja.Lazima sasa wafanye kazi kwa Malengo.Wakumbuke "kuna kuzeeka".Ni muhimu kila bendi ikawa na Vikosi Viwili vya Bendi,cha pili kiwe kikosi cha "under 20"!Mnajua nimekusudia kuzungumzia nini.Lakini,pia,wakati sasa umefika kwa bendi zetu,kujifunza,kutoka kwa magwiji wa muziki wa dansi barani afrika,Franco wa Ok jazz,pamoja na Tabu Ley wa Afrisa Internationale!Kuanzia nidhamu ya kazi ya muziki,Nidhamu na Uhodari wa kulivamia Jukwaa(wacheza show na wanamuziki walio mstari wa mbele "frontliners"),Uvaaji nadhifu wa Kibendi wawapo jukwaani(sio huyu kavaa Tshirt ya blue,mwingine kavaa Jacket la Mvua,mwingine kapiga Kanzu,mwingine kavaa KK,na kadhalika);wanamuziki wasilewe kupita kiasi wawapo jukwaani;na Uniformity katika mambo yote wawapo jukwaani,nk....LAKINI,muhimu zaidi,waondokane na dhana ya kutegemea zaidi "Mapato ya Mlangoni(gate collection)"kwa ajili ya kuboresha na kuendesha maisha yao ya kila siku.Wapo Wataalamu wengi hivi sasa hapa nchini wanaoweza kuwasaidia kwa Ushauri,mfanye nini.Wakati sheria ya Copyright ikiwa inatiliwa mkazo,bendi zenyewe zinatakiwa kuwa na vitengo vya ufuatiliaji wa kazi zao sokoni.Ni vizuri kibiashara,kwanza,bendi itangulie "kutoa au ku shoot video ya wimbo mpya inaotaka kuutoa sokoni",baada ya kupata mrejesho(feedback)kutoka kwa wadau na wapenzi wao,ndipo,bendi itoa Audio CD au recording ya Wimbo wao!Kwa njia hiyo,Audio itanunulika zaidi,kutokana na advertising iliyofanywa na Video yao.Ni ushauri tu.Angalau,bendi itoe Album moja kwa mwaka!Album iliyoshiba na kushibika,ambayo itaweza kutamba hata kwa miaka mitano mbeleni,kutokana na uzuri na umahiri wa tungo na ala zake!kuliko pupa ya kutoa album tano kila mwaka,na zote zisifanye vizuri katika soko.Nina ushauri "Kapu Zima"hapa.Iwapo wadau au wanabendi wataona ni ushauri waliouhitaji,wanipe mrejesho,ili niweze kupakua ushauri zaidi kutoka kwenye Kapu langu!otherwise(utajuaje kama nimesoma,tehe tehe tehe..kwikwi!),nawatakia wote heri ya Krismas na Mwaka Mpya wenye baraka tele!
ReplyDelete