Ndugu watanzania woote muishio Ufaransa na nchi jirani, hata wale mlioko nyumbani mnaalikwa katika sherehe ya kuadhimisha miaka 51 ya uhuru wa Tanzania bara.

Ujumbe huu ukikufukia tafadhali mpashe habari (mjuze) na jirani yako.

Sherehe hii itafanyika tarehe 16/12/2012. Siku ya jumapili kuanzia saa nane, 8 mchana (14:00) Mnaombwa kuzingatia muda ili nanyi muweze kuwa na muda wakutosha kujuzana hili na lile huku kinywaji kikitembea baada ya mlo.

Tutakuwa katika mtaa wa:

7 rue des Galons, 92190 MEUDON, nje kidogo ya jiji la Paris. Tahadhari: Hapa sima-anishi wimbo ule wa Mmbaraka Mwinshekhe. Mtaa huu wa saba nikweli.

Ujumbe wa mwaliko huu unakufikia toka kwa balozi wetu Begum TAJ akiupenyeza kwetu kupitia Ms. Delly Makombe, ambaye ni mwenyekiti wa Jumuiya na chama cha Watanzania waishio Ufaransa (CCWU) akishirikiana kwa karibu sana na katibu dada Pamella A.

Ili kunogesha zaidi shughuli hii, tafadhali tunaombwa soote hasa watakao weza ku-udhuria shughuli hii, tusisahau pendekezo na OMBI lililomo ndani ya barua pepe tulizotumiwa, kama mjuavyo tena tupo katika nchi maarufu inayozalizalisha wine, vin kwa wingi.

Jamani watanzania wooote mnaombwa kuudhuria kwani umoja ni nguvu. Lakini pia ikiwa wakati huu tunakaribia kumaliza mwaka 2012 (Civil year-année civile).

Balozi wetu atapenda tufahamiane zaidi na tujuzane hili na lile katika kufahamu ni vipi mwaka huu unaishia na tunajipanga vipi kukabiliana na changamoto za mwaka ujao, 2013, katika bara lililo na changamoto nyingi hasa mtikisiko na msukosuko wa ki-uchumi.

Wow! Habari zilizonifikia hivi punde ni kuwa, hakika balozi wetu naye atakuwepo ndani ya nyumba.

Hii pia ni fursa yakufahamiana na watanzania wenzetu ambao pengine niwageni wakiwemo wanafunzi, wafanyabiashara, wafanyakazi, nasisi wengine wooote tunaoishi hapa. Njooni tuzungumze. DIASPORA ndiyo sisi. Tupange mipango yakuendeleza umoja wetu na hatimaye nchi yetu. Wakati ndiyo huu.

Chakufurahisha zaidi ni kuwa DJ wetu maarufu ajulikanaye kama Augustino, a.k.a Tino atakuwa akitudondoshea vitu maridadi na murua kabisa kutoka pale nyumbani Tanzania-na Afrika kwaujumla.

DJ Tino nimaarufu sana katika kumbi za burudani hasa ukiulizia shughuli zinazoandaliwa navijana kutoka Africa ya Mashariki, kati na kusini, kaka Tino anavuma hapa. Hasa Watani wetu ambao idadi yao hapa Ufaransa si haba, walao inatuzidi wao humvulia kofia.

Haya nakutakia kila la heri katika maandalizi ya safari yakuja kujumuika nasi. Uwepo wako ndiyo mafanikio ya shughuli hii.

Haya ni mimi ndugu yenu wa Francophonie, 
tawi la Ufaransa 
Frédéric Meela. 

Alamsiki na Mola awajaalie.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...