Mwanamuziki nyota wa dansi kutoka nchini DRC-Kongo,Koffi Olomide akiwasalimia baadhi ya mashabiki wake waliofika kumlaki usiku huu mara baada ya kuwasili akiwa sambamba na skwadi lake zima la Quartier Latin kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA),tayari kwa onesho lake litakalofanyika siku ya jumamosi ndani ya viwanja vya Lidaz Club,Kinondoni jijini Dar na jumapili jijini Mwanza ndani ya uwanja wa CCM-Kirumba,onesho hilo ambalo limedhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) kupitia kinywaji chake cha Tusker kiingilio chake kimepangwa kuwa ni shilingi 10,000/= kwa kichwa kama tiketi ikinunuliwa mapema na shilingi 15,000/= getini.Pichani kushoto ni Mwenyeji wake kutoka kampuni ya Prime Time Promotions Ltd,Godfrey Kusaga
Watangazaji wa Clouds FM na Clouds TV pichan shoto ni Millard Ayo na Ben Kinyaiya pichani kulia wakifanya mahojiano mafupi na Mwanamuziki Koffi Olomide mara baada ya kuwasili usiku huu  kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA),jijini Dar.Koffi alitanabaisha kuwa yeye amekuja nchini Tanzania kwa mara nyingine tena kuwaburudisha na kuwaonesha vipaji alivyo navyo sasa ndani ya kundi lake la Quartier Latin. 
 Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group,Joseph Kusaga akimlaki (mgeni wake) ,Mwanamuziki nyota wa dansi kutoka nchini DRC-Kongo,Koffi Olomide mara baada ya kuwasili kwenye hoteli ya Serena,jijini Dar usiku.Mwanamuziki huyo machachari awapo jukwaani ameshuka na skwadi lake zima la Quartier Latin  kwa ajili ya kutumbuiza siku ya jumamosi ndani ya viwanja vya Lidaz Club,Kinondoni jijini Dar na jumapili jijini Mwanza ndani ya uwanja wa CCM-Kirumba,ambapo kiingilio kimepangwa kuwa ni  shilingi 10,000/= kwa shilingi 15,000/= getini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group,Joseph Kusaga akizungumza na (mgeni wake) ,Mwanamuziki nyota wa dansi kutoka nchini DRC-Kongo,Koffi Olomide mara baada ya kuwasili kwenye hoteli ya Serena,jijini Dar usiku huu.
 Baadhi ya wanamuziki wa Koffi Olomide wakishuka kwenye gari kwenye viunga vya hoteli ya Serena usiku huu.
 Baadhi ya wadau na wapenzi waliokumbana uso uso kwa na mwanamuziki Koffi Olomide usiku huu,wakipata picha ya pamoja.
 Mdau Idd Janguo nae alipata picha ya ukumbusho na Koffi Olomide,ambaye anasema amejipanga vyema kuwaburudisha wakazi wa jiji la Dar siku ya jumamosi ndani ya vuwanja vya Lidaz Club.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...