![]() |
Ngassa |
Akizungumza na Shaffih Dauda, Sheikh Idrissa amesema timu ya El Merreikh imeshakubalina kimsingi na vilabu vya Azam FC na Simba SC na mchezaji na kilichokuwa kimebakiwa na kutia saini kwa mikataba pamoja na kufanya vipimo vya afya ili mchezaji huyo aweze kujiunga na timu hiyo tajiri ya Sudan, lakini muda mfupi baada ya kufika Dar es Salaam mchezaji huyo amekuwa mafichoni - akiwa hapokei simu na muda mwingine anazima bila kutoa taarifa zozote kwa vilabu husika.
“Mrisho Ngassa tulikuwa tumeshafanya nae mazungumzo vizuri na tukakubaliana na ikabakia kumalizana na vilabu vya Simba na Azam, lakini sasa tukiwa tayari tumemalizana na vilabu mchezaji mwenye amekuwa akifanya vitendo visivyo vya kistaarabu, simu yangu hapokei na muda mwingine anaaizima kabisa. Hili sio jambo zuri kabisa kwake na kwa mpira wa Tanzania kiujumla. Anaharibu sifa ya wachezaji wenzie wa kitanzania, ni vizuri angepokea simu na kutueleza kama dili linawezekana au tofauti, kuliko kutuacha sisi tukipoteza muda kuwepo hapa Tanzania. Kwa tabia hii ya Ngassa tumefikia maamuzi ya kwamba mpaka kesho asubuhi kama mchezaji atakuwa hajapatikana then tutasitisha uhamisho wa mchezaji huyu na kuangalia sehemu nyingine mbali na Tanzania.” - Alimaliza Sheikh Idrissa.
Taarifa zilizoenea ni kwamba Ngassa hataki kwenda El Merreikh baada ya kushawishika ili aendelee kuwepo Simba mpaka mkopo wake utakapoisha mwakani na aweze kujiunga na klabu yake ya zamani ya Yanga.
![]() |
Niyonzima |
Baada ya utafiti wa kina, Globu ya Jamii inaweza kuthibitisha kwamba Mrisho Khalfan Ngasa ameshasaini kuchezea Yanga mara tu baada ya mkataba wake na Azam FC kumalizika miezi sita ijayo.
Vile vile imebainika kwamba Kiungo mchezeshaji wa kimataifa wa Yanga, Haruna Niyonzima, ambaye pia alitakiwa na klabu hiyo ya Sudan, naye ameshamwaga wino wa kuchezea Yanga, akikazia mkataba wake wa awali wa kuchezea klabu hicho cha Jangwani. Hivi tunavyoongea yuko mjini Misenyi, Rwanda, kuhudhuria sherehe za harusi za nduguye, alikoenda baada ya kusaini mkataba huo mpya.
Yaani hapo refa kiziwi, laizimeni kipofu.
ReplyDeletekama kweli dogo ngasa hataki kwenda sudan, basi kichwa chake kina upungufu; hivi simba na yanga kuna nini cha maana, mshahara wenyewe hauna uhakika. NENDA SUDAN DOGO HAYO NDIO MAENDELEO OOOOOOOOOOO.!!!!!!!!!!!
ReplyDeleteUmefika wakati wa mpira wa TZ kwenda kitaalamu zaidi na wachezaji inabidi wawe na mameneja. Kwa sasa sijui nana anawashauri hasa ukizingatia maisha waliokulia na elimu waliyonayo. Mshahara wa El Mereikh kwa mchezaji ulikuwa ni USD 4,000 kwa mwezi ambazo ni TZS 6,400,000, kwa miaka miwili ingekuwa TZS 154M pamoja na signing fee ya USD 50,000 (TZS 80,000,000) sidhani kama kuna timu ya TZ inayoweza kulipa hivyo hasa ukizingatia uswahili tunaoona kila siku kuanzia TFF hadi vilabu. Pia kuna faida ya kucheza mechi kubwa ktk ligi ya mabingwa wa Africa. Sijui mchezaji kama kafikiria faida hizi zote na bado akaona ni bora kubaki nchini. Kwa tabia hii ambayo inachangiwa kwa kiasi kikubwa na unazi wa viongozi wa TFF sidhani kama mpira wetu utabadilika.
ReplyDelete
ReplyDeleteNgassa kanishangaza sana kutokea kwenye udaku aisee kaji shusha hadhi balaaa
Sudan AMANI zero! Mtu utoke Tanzania uende Sudan, haujitaki!
ReplyDeletekwa kweli mimi simlaumu anazo sababu zake kwa nini hataki kwenda huko viva Yanga
ReplyDeleteNgassa wewe ni mtu mzima ujuaye unayoyafanya.. Ifike wakati hata wachezaji wathaminiwe coz nakumbuka usajili wake Simba ulikuwa wa kibabe bila ridhaa yake wakati ana uhuru wa kuchagua.. Bwana Ngassa mdogo usimsikilize mtu fanya uonalo litakunufaisha maishani mwako!!!
ReplyDelete