Mkurugenzi wa Uendelezaji wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), David Shambwe akitangaza katika mkutano na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, muda wa kuanza kuuza nyumba 290 za bei nafuu zinazojengwa Kibada, Kigamboni, zitakazoanza kuuzwa Januari 2, mwakani. Kulia ni Meneja Masoko na Utafiti wa NHC, Itandula Gambalagi.
Waandishi wa habari wakiwa kazini wakati wa mkutano huo uliofanyika leo NHC Kanda ya Kinondoni
David Shambwe ( wa Pili kulia) akifafanua jambo katika mkutano huo. Kutoka kushoto ni Muungano Saguya ambaye ni Corporate Social Responsinbility Manager, Meneja wa Mkoa wa NHC Kanda ya Kinondoni, Erasto Chilambo na Meneja Masoko na Utafiti wa NHC, Itandula Gambalagi.
Shambwe akiendelea kujibu maswali mbalimbali ya wanahabari
KAMA KUNA MTU ANAJUA BEI YA NYUMBA INA RANGE KIASI GANI ATUJULISHE
ReplyDeleteMasharti ya kununua/mnunuaji ni yapi? (Of Course ni lazima uwe na pesa, lakini kuna ni Mortgage au cash?)Na kama cash (I doubt)deposit ni kiasi gani? Au Mortgage, deposit ni kiasi gani? Taf toa maelezo kwenye blog kabla ya tar hiyo. Na wadau wa ughaibuni wakitaka kununua masharti ni nini na wao? Maana tunao ndugu zetu huho Ughaibuni wanataka kujua pia. Shukran.
ReplyDeletehivi price ni siri!?,yani mkutano wote huo hakuna swala price nashindwa kuelewa
ReplyDeletenashindwa kuelewa tuwekeeni bei mnaficha nini,
ReplyDeletebei haitajwi hadharani, kwa wengi, "si bei nafuu" hata kidogo!bado tuna safari ndefu sana.
ReplyDeleteVipi mbona ilikuwa rahisi kuwaita waandishi wa habari na kuweka kwenye mtandao tarehe ya kuuza nyumba hizo, inakuwaje vingumu kujibu maswali ya wadau kuhusu bei n.k. Haina haja kutueleza tarehe ya manunuzi wakati bei hatujui, eti 'bei nafuu" kiasi gani? Weka kwenye mtandao kabla ya siku
ReplyDelete