Ukiangalia katika picha hii utawakumbuka watoto hawa Nyambuli Mganga (5) na Gozbert Bwere (3) kutoka mkoani Mara ambao walikuja jijini Dar es salaam na kikundi cha ngoma za asili kutoka mkoani humo, kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 51 ya Uhuru wa Tanzania Bara yaliyofanyika kwenye uwanja wa Uhuru, watoto hawa walitia fora sana mbele ya Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. Jakaya Kikwete na wageni mbalimbali kutoka nje na ndani ya nchi waliohudhuria katika maadhimisho hayo.

Shughuli kubwa iliyofanywa na mtoto mdogo Gozbert Bwere (3)katika upigaji wa ngoma ndiyo iliyowafanya baadhi ya viongozi wa kisiasa na Serikali kuenda kumtunza mtoto huyo, ambapo Katibu wa Itikadi na Uenezi wa NEC CCM Nape Nnauye na Katibu Mwenezi wa chama hicho Mwigulu Nchemba walienda na kumtunza mtoto huyo kwa umahiri wake katika kupiga ngoma.

Jana nilipita maeneo ya Manzese katika moja ya kiota cha siku nyingi Frieds Coner na kumkuta mmoja wa wanakikundi akiwa na watoto hao nje ya hoteli hiyo,akajitambulisha kwamba yeye ni Mpalala Mwendwa na ni msaidizi wa Afisa Utamaduni wa Mkoa wa Mara akaongeza na kusema yeye amefuatana na kikundi hicho kama mmoja wa viongozi wa msafara kutoka mkoani Mara.

Kilichinisikitisha sana ni kiongozi huyo kuonekana akiwa ameshika chupa ya pombe kali aina ya Value akionekana kuwanywesha watoto hao pombe hiyo kwa kifuniko cha chupa hiyo, huku mtoto Gozbert Bwere akikunja sura mara baada ya kunywa pombe hiyo ikiwa ni kuashiria kwamba hawezi kumudu kuinywa.

Kitu kilichiniumiza sana nilipoongea na Bwana Mpalala Mwendwa aliniamba kuwa wazazi wa watoto hao wamebaki Musoma.

Hivyo watoto hao wako chini ya uangalizi wa kikundi hicho pekee jambo ambalo si jema na kuna uwezekano mkubwa wa kumomonyoka kwa maadili ya watoto hao, kwani hawana ulinzi wa kotosha kama ilivyoshuhudiwa jana wakiwa wananyweshwa pombe hiyo ya Value na kiongozi huyo.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa NEC CCM Nape Nnauye na Katibu Mwenezi wa chama hicho Mwigulu Nchemba wakirejea jukwaani mara baada ya kuwatunza watoto hao Nyambuli na Gozbert wakati wakicheza ngoma katika maadhimisho ya miaka 51 ya Uhuru wa Tanzania Bara kwenye uwanja wa Uhuru.
Mtoto Gozbert Bwere (3) akionyesha uwezo wake katika kupiga ngoma huku akiwa amelala chini katika maadhimisho hayo.
Mtoto Gozbert Bwere (3) akifanya vitu vyake katika kupiga ngoma katika maadhimisho hayo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. Lakini unakubali hapotoshi Bunge hili kwa kuchanganya mambo ya kurithi na Mswada huu? Yeye anasema kwamba mtu akiwa na wanawake wawili, watoto ... DB Mall

    ReplyDelete
  2. Please, Issa Michuzi I beg you to help these kids. This is really sad. Hawa watoto ni wadogo sana, kama hao wacheza ngoma wameanza kuwanyeshwa pombe, si bure kuna mambo mengine wanawafanyia hawa watototo. Chonde chonde Bw. Michuzi naomba uwasaidie.

    ReplyDelete

  3. Tufanye linalowezekana, waheshimiwa wamewaona na kuwatunza isiishie hapo!!!

    Protect these children PLEASE!!!

    ReplyDelete
  4. hiyo ni exploitation watoto wanatakiwa kucheza na watoto wenzao si kuwakuza kabla ya wakati wao watapata matatizo ukubwani wa ku-adjust na society

    ReplyDelete
  5. hivi ni kuwatunza au kuwatuza?

    Maana kuwatunza ni kuwasaidia, kuwalea na kuwapa sehemu ya kula na kulala. Chakula, mavazi na malazi.

    Kuwatuza ni kuwapa zawadi.

    nisaidieni jamani waosha vinywa.

    ReplyDelete
  6. Where are you the Honourable mama Simba, this issue falls directly under your portfolio!!

    ReplyDelete
  7. Hili afisa utamaduni la mkoa ndo anawafundisha watoto hawa utamaduni wa Musoma?

    ReplyDelete
  8. thank you for showing concern over these kids, ila haitoshi tu kutupa post hii kama hukuweza fanya lolote la kusaidia. Kuona akinywesha pombe na kulifumbia macho halitoshi. Other wise ni busara zaidi kulifikisha kwa wahusika.
    Pili, viongozi wa NEC sii viongozi wa serikali. hawa ni viongozi wa chama. tujitahidi kuwa makini katika kutoa taarifa

    ReplyDelete
  9. Nashukuru sana kwa taarifa bwana Issa Michuzi na tunashukuru sana kwa mwenyezi mungu kuweza kukusaidia wewe kufika eneo hilo na kuona kinachafanyika dhidi ya hao watoto. Sasa na wewe kama mzazi au umeguswa na hili Je mwanzo wa kulitatutu hili umeufanya? twashukuru kwa kuweza kutufahamisha maana kwa wale wenye kuguswa pia watachangia hili katika kunusuru maisha ya watoto hao. naomba muongozo uanzie kwako Bwana Michuzi ili iwe rahisi kwa wengine kujua watafikisha wapi au watawapata vipi watoto hao ili kuweza kuwanusuru. ni watoto wenye kipaji ila inasikitisha wamekosa malezi. Ewe mola tusaidie waja wako hatujui tulitendalo. Maana huyo anayewafanyia hao watoto hivyo si dhani kama ana mtoto/ watoto na angeweza kufurahi aku kuruhusu watoto wake kufanyiwa kama anavyofanya.

    Issa usiliachieee hili hujui kesho akhera umeandaliwa nini waokoe watoto hawa kwa njia zote uzijuazo. na Je wengine wanaotaka kutoa msaada kwa watoto hao watapitia wapi?

    ReplyDelete
  10. Mimi kama mzazi nimeumua mno siwezi hata kuelezea. Please the responsible authorities saidieni hawa watoto.

    Mama Simaba please!!!!! MUNGU WANGU TUSAIDIE.

    ReplyDelete
  11. UWIII!!!!!huu ni unyama usiovumilika mbele ya jamii.ndugu yetu asante kwa taarifa.Je ulichukua hatua gani za awali kuwanusuru na unyama zaidi ambao unaweza kuwapata malaika hawa?Eeh taifa lenye amani matendo haya ni matokeo ya sherehe nje ya uwanja wa uhuru yasiyo rasmi.Wahusika na maandalizi ya sherehe rasmi tuambieni wazazi ahadi zenu mlivyotekeleza na usalama wao.Kiongozi wa kundi hili awajibishwe kisheria na unyanyasaji huu,tena ni mwizi kwani fedha walizotunzwa atakuwa amewarubuni kuwahifadhia na sasa ndio matanuzi jijini hayo hapo dhahiri bila kificho.Nasi wazazi hivi kweli mtoto wa miaka mitatu bado ananyonya unamucha na mifisi kama hii umbali wote huo Musoma hadi Dar kwa kipindi kirefu hivyo?Hamsikilizi vyombo vya habari na unyama unaoongelewa kila uchao?Wanaharakati ondokeni maofisini na kutuonyesha vitendo adilifu kwa jamii.OKOA OKOA OKA tafadhalini,nimechanganyikiwa mzazi mwenzenu.

    ReplyDelete
  12. waacheni watoto wapige kikali wapate stimu hivi mnajuwa kuwa hata huko kijijini huwa wanapiga tembo au mnazi?

    viongozi waliwatuza na kufaidika na burudani hiyo je walitoa msaada gani au muongozo gani ili kuwaongoza hao watoto? kwa kuwasaidia kukuza vipaji vyao?

    alaaa wacheni kuchonga sana kama mnauwezo wa kuchonga chongeni kwa viongozi wenu wabovu.

    ReplyDelete
  13. mkuu wa mkoa wa Mara na uongozi wa mkoa kwa ujumla chukuen hatua zinazostahili kwa huyu ofisa kwani huu ni ukatili mkubwa dhidi ya watoto ambao hawajui kitu.

    ReplyDelete
  14. Huyu Afisa Utamaduni achukuliwe hatua kaaali sana iwe fundisho kwa hengine

    ReplyDelete

  15. WEWE ANON WA 11:57:00 AM

    NYINYI NDIO MNAOWANYWESHA WATOTO WENU POMBE, HALAFU WAKIJA KUWA MATEJA WA POMBE UKUBWANI WATU TUNASHANGAA.

    JINGINE WEWE SHADIDIA TU UNDERAGE ALCOHOL CONSUMPTION, SUBIRI WATOTO WAKO WAKULETEE UNDERAGE MIMBA ZINAZOTOKANA NA ULEVI

    ReplyDelete

  16. Anon wa Dec 12, 11:57:00 AM

    UMEJIFUNGA MSULI HADHARANI, MSULI UNAANGUKA, BADALA YA KUCHUTAMA WEWE UTAINAMA KUUOKOTA.

    ReplyDelete
  17. Jamani jamani mithupu tujuze maendeleo ya makinda haya jamani.Zijulikane kwanza thamani ya waizotunzwa kwa makadirio halafu pia masurufu aliyokabidhiwa na mkoa,naamini hata wazazi walichangia matunzo ya ziada kwao.Kisha basi hatua za kinidhamu na hitimisho la kumwajibisha tuzisikie pls mithupu ebu endeleza jambo hili hata kwa msaada wa vyombo vya dola endapo umekwama mbona mambo yote yako hadharani jamani?Hata nawe Nape hujalijua hili hadi sasa Mungu awatangulie katika yote mtayoyaamua yaweze kuwa ya haki na uadilifu.Achieni viti mfike huko Manzese mkukuruke na huyo dhalimu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...