Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika uwanja wa ndege wa Lindi mara baada ya kuwasili mkoani Lindi asubuhi hii ambako anahudhuria maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani yanayofanyika Kitaifa kwenye uwanja wa Ilulu mkoani humo, wadau mbalimbali wanaojihusisha na masuala ya kupambana na ugonjwa wa ukimwi wamejitokeza na kushiriki katika maonyesho hayo yenye lengo la kuelimisha na kukumbusha juu ya hatari za ugonjwa wa ukimwi na mbinu mbalimbali za kupambana nao.Watatu kulia ni Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete na kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Lindi,Mh. Ludovick Mwananzila.Kauli mbiu ya mwaka huu ni
"Tanzania Bila Maambukizi mapya, Unyanyapaa na vifo vitokanavyo na Ukimwi Inawezekana".
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Waziri wa Afya na Ustawi wa jamii Mh. Hussein Mwinyi mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Lindi Mkoani.katikati ni Mh. William Lukuvi Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu , Sera na uratibu wa bunge
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Lindi mjini,Mh. Salum Barwany wakati alipowasili mjini Lindi asubuhi hii kwenye uwanja wa ndege wa Lindi.
Viongozi mbalimbali wakimlaki Rais Jakaya Kikwete kwenye uwanja wa ndege wa Lindi leo asubuhi hii.PICHA NA FULLSHANGWEBLOG.COM

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Tatizo ni Rais ana chagamoto na credibility.Kuhusu madawa na experiment kwa wagonjwa wa AIDS kwenye Jiji la Dar.Kama watalamu wake wameona necessary kwa Rais kupiga picha na Albino wakati uko Lindi basi wali kuwa wana fahamu kwamba mambo ya Uwaji wa Albino watu wegeneo wana amini una husiana na watu karibu na uongozi wake.Kwa nini Rais alifikiri kwamba akenda Lindi siku ya AIDS ita accomplish nini? Wakati serikali yake ni responsible kwenye tatizo la AIDS Dar? Kama siyo chuki basi nini?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...