
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akishuhudia utiaji saini mkataba wa kusaidia Mpango wa kupiga vita ukimwi nchini Tanzania.Pichani Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu ndugu Peniel Lyimo,Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Ndugu Ramadhani Kija na Mkurugrnzi wa Global Fund Dr.Christopher Ben Wakitia saini Mkataba huo ambapo Global fund itatoa jumla ya Dola za Kimarekani milioni Mia tatu na nane (308 U S $) kwaajili ya Tanzania.Utiaji Saini Huo ulifanyika leo katika wanja wa michezo wa Ilulu yaliukofanyika maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani.Wengine wakishudia Utiaji saini mkataba huo ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete,Wziri wa Afya Dr.hussein Mwinyi na Bi Ursula Muller Mjumbe wa Bodi ya Global Fund
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiinua juu kitabu kuzindua rasmi mpango wa Kutokomeza maambukizi ya Ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto(Prevention From mother To Child Trsnsmission(PMTCT) wakati wa maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani yaliyofanyika katika uwanja wa michezo wa Ilulu mjini Lindi jana. Wengine katika picha ni mke wa Rais Mama Salma Kikwete(kulia),Waziri wa Afya Dkt.Hussein Mwinyi(wanne kushoto), Mkurugenzi wa Global fund Dkt.Christopher Ben(kushoto) na wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bwana Ludovic Mwananzila
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...