Rais Jakaya Mrisho Kikwete (kulia) akipokea ujumbe wa wasanii wakongwe wa muziki wa dansi pamoja na filamu kutoka kwa Kiongozi wa Wasanii hao,Waziri Ally (aliesimama) wakati ujumbe huo ulipomtembelea Ikulu jijini Dar es salaaam leo kwa kumshukuru Rais kwa kuwajali wasanii wa aina zote na hata kuamua kutoa tuzo kwa wasanii.ambapo mwaka huu amewatunuku Muhidin Maalim Gurumo na Hayati Marijani Rajabu.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete (kulia) akiwa katika mazungumzo na Kiongozi wa Band ya Kilimanjaro,Waziri Ally alieambatana na ujumbe wa wasanii wakongwe wa muziki wa dansi pamoja na filamu,Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na ujumbe wa wasanii wakongwe wa muziki wa dansi pamoja na filamu uliomtembelea leo Ikulu jijini Dar es salaaam kwa kumshukuru kwa kuwajali wasanii wa aina zote na hata kuamua kutoa tuzo kwa wasanii.ambapo mwaka huu amewatunuku Muhidin Maalim Gurumo na Hayati Marijani Rajabu.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa wasanii wakongwe wa muziki wa dansi pamoja na filamu uliomtembelea leo Ikulu jijini Dar es salaaam kwa kumshukuru kwa kuwajali wasanii wa aina zote na hata kuamua kutoa tuzo kwa wasanii.ambapo mwaka huu amewatunuku Muhidin Maalim Gurumo na Hayati Marijani Rajabu.PICHA NA IKULU.


Serikali imeanza kutoa Nishani kwa wasanii kwa vile inatambua umuhimu wao katika jamii.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete amewaeleza wawakilishi wa sanaa mbalimbali nchini waliofika Ikulu leo asubuhi kutoa shukrani kwa Mheshimiwa Rais kwa kuwatambua na kuwapa heshima kubwa ya Tuzo na Nishani wasanii katika siku ya sherehe za Uhuru za tarehe 9 Disemba, Ikulu, Dar-Es-Salaam.
“Tumetoa Nishani kwa vile wasanii wanatoa mchango mkubwa, tumeanza kutoa nishani mwaka huu na tutaendelea kutoa miaka ijayo kwani kwa kuitambua sanaa, mnawapa moyo wasanii kuendelea kujituma na kuwa wabunifu zaidi” Rais amesema na kuongeza, “Tumeingiza Nishani ya Wasanii na Watafiti maana nao wanafanya kazi kubwa sana ya kutafiti mazao na mbegu mbalimbali ambazo zinaongeza tija katika kilimo nchini”.
Katika kumbukumbu ya kusherehekea miaka 51 ya  Uhuru wa Tanzania bara mwaka huu, Rais Kikwete alitunuku nishani kwa makundi mbalimbali ya watu waliotoa mchango mkubwa katika jamii na waliotumikia taifa kwa uadilifu.
Rais alitoa Nishani ya Sanaa na Michezo kwa mara ya kwanza kwa wasanii nchini ambapo Bi. Fatma Baraka Khamis (Bi Kidude) kupitia Baraza la Sanaa Zanzibar, Kiongozi wa Muziki wa Dansi ya Msondo Ngoma Muhidin Gurumo, Kiongozi wa Zamani wa Bendi ya Dar Intrenational Marehemu Marijan Rajab walipata tuzo hiyo.
Wengine ni Msanii wa maigizo na filamu nchini Marehemu Fundi Said (Mzee Kipara) na Mwanariadha mkongwe John Steven Akwari.
Rais amewataka wasanii kushirikiana na serikali lakini pia wawe mstari wa mbele katika kupigania haki zao na sio kusubiri serikali tu iwafanyie hivyo.
Wasanii hao wamefika Ikulu wakiongozwa na Bw. Ruge Mutahaba wa Clouds Media Group.
Wengine ni Addo Mwasongwe, Rais wa Shirikisho la Muziki na Mwenyekiti wa Chama cha Muziki wa Injili, Bw. Juma Ubao Mwenyekiti wa Chama cha Muziki Tanzania (CHAMUDATA).
Bibi  Shakila Said, Mkongwe wa Muziki wa Taarab Nchini, Bi Carola Kinasha Msanii wa Muziki , Mzee King Kiki msanii wa Muziki wa Dansi Mwana FA, msanii wa Kizazi Kipya na Bw. Waziri Ally , msanii wa Muziki.
Wawakilishi hao pia wamemshukuru Rais kwa msaada wa hali na mali anaotoa kwa wasanii mbalimbali wanapopata matatizo ambao hivi sasa wapo katika hatua mbalimbali za matibabu ya afya zao hapa nchini na nchi za Nje.
“Haya mengine ninayafanya tukama wajibu wa  kibinadamu kwa vile nina nafasi ya kufanya hivyo na pale tunapokua na uwezo tunasaidia kama binadamu wenzetu” Rais Amesema.

Imetolewa na Premi Kibanga,
Mwandishi Habari wa Rais, Msaidizi,
Ikulu - DSM
21 Desemba, 2012 



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hongera sana wasanii wetu kwa kwenda kumshukuru ndugu rais kwa mchango wake kwenu,ila na swali langu ni hili ktk picha namuona Ruge Mutahaba yeye alienda kama nani?! maana siyo mwanamumuziki naomba ufafanuzi wadau

    ReplyDelete
  2. Alienda kama mdau

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...