Marehemu Amina Singo enzi za Uhai wake.

Shrikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha aliyekuwa mtangazaji wa habari za michezo katika kituo cha redio cha 100.5 Times FM, Amina Singo kilichotokea usiku wa kuamkia jana.

Msiba huo ni mkubwa katika sekta ya habari na mpira wa miguu kwani kwa nyakati tofauti kupitia taaluma ya uhandishi wa habari, Amina alifanya kazi na TFF, hivyo mchango wake katika mpira wa miguu tutaukumbuka daima.

Tutamkumbuka kama mtangazaji wa habari za mpira wa miguu na michezo kwa ujumla. TFF tunatoa pole kwa familia za marehemu Amina Singo, ndugu, jamaa na marafiki na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.

Mungu aiweke roho ya marehemu Amina Singo mahali pema peponi.

Amina

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Kweli kifo hakina huruma jamani du!! Binti mrembo huyu kaondoka!! Mungu ailze roho yake mahali pema peponi.Pole kwa ndugu jamaa na marafiki wote.Bwana alitoa na bwana ametwaa Jina la Bwana na lihimidiwe.

    ReplyDelete
  2. Imauma sana ila mwisho wa siku hatuna ujanja pindi tuondokewapo na wapendwa wetu. Mungu ni mwema na maamuzi yake ni sahihi siku zote. Wafiwa, poleni sana!

    ReplyDelete
  3. Kwa kweli inauma sana. Kifo kikija wakati mtu bado hajafikia malengo yake na bado familia na taifa vinamtegemea, inauma zaidi. Mimi nimpe pole boyfriend wake!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...