KAMPUNI ya Lakeland Africa kesho itaanza safari ya ‘Mtanzania tembelea Tanzania’ kwa siku 14 kwa lengo la kukuza utalii wa ndani na kujenga utamaduni wa Watanzania kutembelea vivutio vya utalii nchini.

Safari hiyo itakayoanzia Mlimani City Dar es Salaam kesho inatoa fursa kwa watanzania kutembelea vivutio mbalimbali ikiwemo Hifadhi ya Saadan, Pangani, Lushoto, Tarangile, Olduvai Gorge, Lake Manyara, Ngorongoro na Serengeti na pia watapata nafasi ya kutembelea kijiji cha Butiama alikozaliwa Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Nyerere na kuzuru katika kaburi lake.
 
“Lakeland Africa sasa itaendesha safari za namna hii kuhimiza watu kutembelea vivutio vya utalii nchini kwa kauli mbiu ya ‘kuwa mtalii ndani ya nchi yako”
 
Kuanzia mwezi januari mwakani Lakeland Africa itaendesha safari za kila wiki kwenda hifadhi na makumbusho ya kistoria katika maeneo mbalimbali hapa nchini ikiwamo Lushoto, Pangani, Saadani, Selous, Kilwa, Bagamoyo na Mikumi
 
Katika kuhakikisha kuwa kila Mtanzania anapata fursa hii ya kuitembelea nchi yake Lakeland Africa imeandaa ratiba ya mwaka mzima ya safari zote ili watu waweze kuchagua na kupanga safari kulingana mahitaji yao.
 
Wapigie Lakeland Africa sasa kupanga safari yako ya mwakani, mwezi wowote utaopenda kuzuru na kuwa mtalii ndani ya nchi yako.
 
Imetolewa na Lakeland Africa.
‘Kuwa mtalii ndani ya nchi yako’

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...