Siku mwanamuziki wa Kizazi Kipya Rehema Chalamila, maarufu kama RAY C, alipomtembela Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete Desemba 10, 2012 Ikulu jijini Dare s Salaam na kumshukuru kwa msaada wa matibabu aliyompatia wakati alipokuwa mgonjwa hivi karibuni.

 Rehema aliyefuatana na Mama yake Mzazi Margareth Mtweve na Dada yake Sarah Mtweve alimweleza Rais kuwa afya yake sasa imeimarika na kwamba muda si mrefu ujao atarejea jukwaani kukonga nyoyo za mashabiki wake. Kwa upande wake, Mama Mzazi wa Ray C amemshukuru Rais Kikwete kwa kuokoa maisha ya mwanaye na vilevile ametoa wito kwa watu wanaokusanya michango kwa ajili ya mwanaye waache kufanya hivyo kwani matibabu ya Ray C yamegharamiwa na Rais.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Ahsante sana Raisi kwa msaada wako,

    Pia ndugu yetu Ray C tunaomba kwa siri utoe orodha ya majina ya wabaya waliokuwa wanakupa hayo Madawa ya kulevya ili sisi Wanaharakati wa Vita dhidi ya Madawa hayo tuweze kukabiliana nao watu hao kwa kuwa wao ndio kikwazo kikubwa kwetu kama unavyoona walivyotaka tukuzike mapema zaidi ya muda aliopanga Mungu.

    Orodha hiyo ifikishe kwa Mhe. Raisi JK kwa siri kubwa na kuwa Raisi atafarijika sana na hatua hiyo akihakikisha ya kuwa umeazimia kubadilika kabisa!

    ReplyDelete
  2. Hongera Raisi JK,

    Lakini kiu yetu ni kutaka tukabiliane na hao waliokuwa wanampimia Madawa Ray C na kumdunga hizo sindano.

    Je, Ray C upo tayari kutupatia listi ya hawa watu ambao ni maadui wa nchi yetu?

    ReplyDelete
  3. Sawa Ray C,

    Isipokuwa Raisi JK na sisi wote tutafarijika zaidi endapo hutorejea tena ktk madawa.

    Pia kama umekusudia kurudi Jukwaani Kimuziki tunaamini utakuwa unatumia chai,maji na soda pia vinywaji vingine vya kawaida na si pombe, na vichangamsho vingine ili kuwa mchangamfu na kutubmuiza badala ya madawa na aina zingine za ulevi au siyo?

    ReplyDelete
  4. Anon wa kwanza kabisa unachosema kinamake sense. Kama Ray C akiri kuwa na tatizo na sasa anapata msaada ambao uko supported na Rais wa nchi basi atoe majina ya watu waliokuwa wanampa hizo dawa.

    It common sense, tutafute chanzo cha tatizo..

    ReplyDelete
  5. Ray C hatakiwi kupewa kazi ya 'Gagula' ya kutambulisha wachawi kwa mda huu. Anachohitaji ni kusahau yote yaliyopita na kuanza maisha upya.

    ReplyDelete
  6. Ni kweili. apeleke taarifa ya siri kwa mheshimiwa rais ili waliompa madawa wakamatwe sababu wanaendelea kuharibu taifa letu

    ReplyDelete
  7. Nyie hamtaki RAY C aendelee kuishi? Hamjui kuwa WAZEE WA MADAWA YA KULEVYA ni MAFIA WA NGUVU? Atakapoanza KUROPOKA tu kwa kuwataja. Au akikamatwa mmojawao, wenzie wakajua, RAY C ataimbiwa tangulia.

    ReplyDelete
  8. I am so happy that our president is such a Mensch!
    Says Gregory.

    ReplyDelete
  9. Kikwete, I could vote you a hundred times. You are the best!

    ReplyDelete
  10. Nani kama yeye, Kikwete. No one like you baba. You are simply the best

    ReplyDelete
  11. Mdau wa 7 hapo juu,

    Hakuna sababu ya kutishana!

    Watu wa Madawa ni wa kawaida na wajinga tu, ni vile wanatumia sana ile udhaifu wa njaa na shida za watu miongoni mwetu ili kufikia malengo yao.

    Nakuhakikishia wanaweza kukamatwa,
    wakafikishwa kwenye sheria na wakaadhibiwa vilivyo kama tutaamua!

    Na wasifanye lolote!

    Wewe mtu mmoja ama genge la watu kadhaa (ikitokea watu waamue) mtashindana na nchi yenye Watu Wazalendo, Utawala na Serikali?

    Acheni masihara!

    ReplyDelete
  12. Wewe No. 7 ...Hamjui kuwa WAZEE WA MADAWA YA KULEVYA ni MAFIA WA NGUVU?...

    AMEFUNGWA SILVIO BERLUSCONI WAZIRI MKUU WA ITALIA BILIONEA NA MTU WA MIPANGO KIBAO ATAKUWA MUUZA MADAWA WA BONGO AU GENGE LA WABONGO WAUZA MADAWA?

    OHOOO!

    ReplyDelete

  13. ANON WA 7 IN MY OPINION IS RIGHT.

    IT IS AN INTENSE NETWORK, DUNIA NZIMA.

    NCHI "TAJIRI" PAMOJA NA MBINU ZAO ZOTE ZA KIKACHERO LIBENEKE LINAENDELEA KAMA KAWAIDA.

    KUJIPA U RAMBO WA "KUJITOKEZA KUPIGA VITA" ETI NAWAJUA, KWA DUNIA YETU HII YA LEO HUFIKI MBALI.

    REMEMBER AMINA.

    CHA MSINGI NI WAZAZI KUWAWAHI WATOTO WETU BADO MAPEMA, KUWAELEZA ATHARI, HATARI NA UBAYA WA HII KITU.

    NA PIA KUWAPA MSAADA WALE WANAOJITOKEZA KUOMBA KUSAIDIWA KAMA HIVI, MAANA PROCESS INAHITAJI GHARAMA KIDOGO.

    NANI KAWEZA?


    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...