Na Sixmund J. Begashe wa Makumbusho ya Taifa
Tamasha kubwa la watoto la sanaa na
Utamaduni linatarajiwa kufanyika Makumbusho na Nyumba Utamaduni kuanzaia tarehe
7 na 8 mwezi huu, ambapo vikundi zaidi ya 10 vya watoto chini ya miaka 15 vinatarajiwa
kushiriki. Hayo yamwesemwa na Mkurugenzi wa Watoto Arts Organization (WAAO)
Bibi Teresia Makene.
Bibi Makene ameelaza kuwa hadi sasa vikundi
vipo tayari na vimejiandaa vyema katika kulipamba Tamasha hilo la Watoto la
Sanaa na Utamaduni, aliongeza kuwa Tamasha hilo litapambwa na Ngoma, Musiki,
sarakasi, ngojera, Mashahiri, Sanaa za Ufundi na Sanaa shirikishi.
Akielezea madhumini ya Tamasha hilo, Bibi
Makene alisema kuwa Tamasha hili litawasaidia watoto kukuza vipaji vyao katika
tasnia ya sanaa na Utamaduni, kuimarika kimaadili yenye kuzingatia mila na
desturi za mtanzania, kuwajengea watoto tabia ya Uzalendo na kuutambua Uridhi
wao kwa kupitia Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni.
Bibi
Makene ametoa wito kwa wazazi wa watoto kuwa wawalete watoto wao kwa wingi
katika Tamasha hili la watoto, na pia Bibi Makene anaendea kutoa wito kwa wadau
mbali mbali kujitokeza na kulisaidia Tamasha hili kwani linamanufaa makubwa kwa
Taifa letu
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...