Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inawatangazia wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na vyuo vya afya nchini kwa mwaka wa masomo 2012/13 kama ilivyotangazwa katika vyombo vya habari, kuripoti vyuoni haraka iwezekanavyo.
Vyuo vilifunguliwa tarehe 12 Novemba 2012 na mafunzo tayari yameanza. Mwisho wa kuripoti ni tarehe 9 Desemba 2012.Baada ya tarehe hiyo nafasi yako itajazwa na mtu mwingine .
Tangazo hili limetolewa na :-
Kaimu Katibu Mkuu
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii
S.L.B. 9083
Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...