Mwenyekiti wa Tanzania Mitindo House na Muandaaji wa Onyesho la Mavazi la Tanzania Red ribbon Fashion Gala,Khadija Mwanamboka (kulia) akikabidhi cheti kwa Mwanamitindo Maarufu nchini,Flaviana Matata ambaye ni Muanzilishi wa taasisi ya kusaidia jamii iliyo kwenye matatizo ya Flaviana Matata Foundation,wakati wa kuadhimisha Miaka Mitano ya Onyesho la Mavazi la Tanzania Red Ribbon Fashion Gala ambalo hufanyika Desemba 1,kila mwaka ikiwa ni kuadhimisha siku ya Ukimwi Duniani,lililofanyika kwenye Hoteli ya Serena,jijini Dar es Salaam jana.

Mwanamitindo Maarufu nchini,Flaviana Matata (kushoto) ambaye ni Muanzilishi wa taasisi ya kusaidia jamii iliyo kwenye matatizo ya Flaviana Matata Foundation akiongoza mnada wa nguo walizozivaa kwa ajili ya kukusanya hela ya kusaidia wahitaji walio chini ya Taasisi hiyo,ambapo hadi mnada wa vitu mbali mbali unamalizika jumla ya shilingi Milioni 72 ziliweza kukusanywa hiyo jana.Kulia ni Mwanamitindo,Jenuffer Bash.
Wanamitindo wakipita jukwaani kuonyesha mavazi mbali mbali yaliyobuniwa na Wabunifu wa hapa nchini.
Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini,Mh. Zitto Kabwe akienda sambamba na Msanii Linex wakati wakiimba wimbo wa Leka Dutigite ulioimbwa na Wasanii mbali mbali wanaotokea Mkoani Kigoma.

KWA MAPICHA KEDEKEDE

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Bwana MICHUZI nikuulize ivi huyu KHADIJA MWANAMBOKA ameolewa .Maana mimi mwenzako nimemuhusudisha sana tuu yaani nimemmaind kama atakuwa yuko single basi tuanze kuwasiliana ili niwasilishe maombi yangu. mimi nausudisha sana magari makubwa.maombi ya ndowa sio kimada cha pembeni.

    ReplyDelete
  2. We mdau acha ulafi, angalia kidole chake cha shada, utalimbwa bure kutamani vya watu!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...