Bw.John Lwande ambaye ni mwenyekiti wa UmojaSwitch akizungumza wakati wa kongamano. Bw.John Lwande aliezea kuhusu mafanikio yaliyofikiwa na UmojaSwitch katika kufikisha huduma za kifedha kwa watu walio mbali na huduma hizi. Alisisitiza jinsi ambavyo UmojaSwitch imeweza kuunganisha benki kama wanachama na wamiliki wa mtandao huo.Akielezea kwamba, mpaka sasa mtandao huo umefanikiwa kuwa na wanachama ambao ni benki 24 zilizopo Tanzania bara na Visiwani.
Kwa sasa mtandao huu unatoa huduma zake kwa kupitia zaidi ya ATM 150 zenye nembo ya Umoja. ATM hizi zimesambaa nchi nzima . Lengo kubwa ni kuwarahisishia wateja wao kupata fedha kokote nchini na kwa bei nafuu, pia kuwafikia wananchi walio katika maeneo ya mbali na huduma za kifedha.Mbali na huduma za kawaida kwa kutumia ATM, UmojaSwitch imeanza kutoa huduma ya “card-less transfer” ambayo mteja anaweza kutuma pesa kwa ATM kadi yake kwenda kwenye namba ya simu yoyote na kuchukua katika ATM ya Umoja bila kadi. Vilevile mteja wa Umoja anaweza kutuma fedha kwenda moja kwa moja kwenye akaunti ya mteja mwingine hata kama mteja huyo yuko benki nyingine kupitia huduma ya “Inter-bank Transfer”.
Mwishoni alisisitizia kwa kusema kuwa, kukosekana kwa mtandao mmoja wa taasisi za fedha ni tatizo la kiuchumi.Hivyo basi, yapaswa kuangalia umuhimu wa jinsi ya kuweka switch ya taifa kupitia mfano wa UmojaSwitch.
Pichani ni Rais Jakaya Kikwete(katikati) akiwa na viongozi mbalimbali kutoka taasisi za kifedha , wakiwemo wanachama wa mtandao wa UmojaSwitch mara baada ya kufungua Mkutano wa 16 wa Taasisi za Fedha katika ukumbi wa AICC, Arusha uliofanyika November 26 hadi 27, 2012.
Bw.Charles Singili akitoa neno la shukrani kwa Rais Jakaya Kikwete baada ya ufunguzi wa kongamano hilo. Bw.Charles Singili ni makamu mwenyekiti wa matandao wa UmojaSwitch baada ya kuwa mwenyekiti tangu 2006 mpaka 2011.
Pichani kulia ni Professa Beno Ndulu (Gavana wa Benki Kuu Tanzania) akiwa pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa UmojaSwitch Bw.Danford Mbilinyi mara baada ya kubadilishana mawazo. Gavana aliipongeza UmojaSwitch kwa kuonyesha njia kuelekea kuunganisha mitandao ya kifedha nchini.
Gavana wa Benki Kuu,
ReplyDeleteMhe. Prof. Ndulu, pana methali kwa lugha ya Kabila la Kizigua inasema 'UKUMWONELA ZUMBE NAHO UKUMLAMSIZA',,,kwa Kiswahili 'MAHALAI UNAPOMWONA KIONGOZI NDIPO HAPO HAPO UNAPOPATA NAFASI YA KUMSALIMIA' !
Sasa nimekuona hapo kwenye picha ya chini nikaona na mimi nichukue nafasi hii kutupa yangu mawili matatu, maana kama kufika kwako pale Minara Miwili BOT inakuwa kaazi kweli kweli pana milango ya kuzunguka na mashine za kupitishwa mwili mzima ili kukaguliwa na maswali kibao kama ,
-Unakwenda wapi?,
-Huyo unamtafuta kwa nini?,
-Una ahadi naye?,
-Unamfahamu vipi? Kwani wewe -
unatokea wapi?
-----------------------------------
MASWALI YANGUA MATANO (5):
-----------------------------------
1.Kama mfumuko wa bei unazaliwa na kupanda kwa gharama za maisha kwa vile vitu muhimu vinavyowagusa wengi ktk maisha 'Basket of Consumer Price Index (CPI)' kimojawapo kikiwa ni chakula, kwa nini bei ya chakula ktk Tanzania inapanda kila uchao wakati nchi haina ukame wala njaa?, huku maghala yakiwa yanavunjika kwa mavuno?
2.Kwa nini bei ya chakula katika Tanzania haina tofauti kati ya shamba kwenye kianzo cha mavuno na masokoni Mijini kwenye soko la walaji?
Mfano bei ya Kilo 1 ya mchele Rujewa au Kyela-Mbeya mchele unakolimwa ni sawa au haina tofauti sana na bei ya Sokoni Dar Es Salaam!
3.Kama Tanzania ina mfumo wa soko huria kwa bidhaa zake, yaani Bei ya bidhaa kuamuliwa na hali ya soko kati ya Mahitaji / na Upatikanaji 'DEMAND AND SUPPLY' ,je pana mwenendo wa kweli kwa bei ya bidhaa za chakula ktk masoko ya Tanzania (tukizingatia huo Mfano huo wa bei ya mchele Kyela-Mbeya na Sokoni Kisutu au Sokoni Kariakoo-Dar Es Salaam?)
4.Kwa nini baadhi ya nchi za Jirani za eneo letu la Afrika ya Mashariki zenye njaa zaidi na 'food insecurity' yaani hatari ya kuangukia kwenye njaa au uhaba wa chakula zina mfumuko wa bei chini kuliko Tanzania?
-Kenya Inflation 6.7
-Rwanda Inflation 5.3
5.Mamlaka yako BOT inachukua msimamo gani kuhusu kudhubiti mfumuko wa bei wa bidhaa za chakula cha nchini (AMBAO KWA DALILI ZA WAZI UNAONEKANA NI BANDIA) hasa za chakula kilichokuwa na sili ya Tanzania zilizolimwa nchini?, hasa kusimamia bei za bidhaa hizo muhimu?
.............................
E-mail:mohamedtzn@AOL.COM