Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Kweli tuwasikilize ila wajue nao wanatumia rasilimali zitokazo kwa wengine, mfano mafuta, umeme nk,,, kwa kujaribu tuwafungie umeme na mafuta waonje j j (joto ya jiwe)

    ReplyDelete
  2. Mh. Zitto,
    Naunga mkono hoja zako. Mikoa ya Lindi na Mtwara ilipuuzwa na kutengwa na serikali za kikoloni na hata huru. Mikoa ile imekuwa hifadhi ya nguvukazi kwa ajili ya sehemu nyingine za nchi. Wanaume wenye nguvu walipelekwa mwenye mashamba na migodi. Wasome wachache wa mwanzo wakapewa madaraka serikalini hivyo wakawa watiifu kwa serikali. Matokeo yake kusini kukabaki maskini hadi leo. Miundombinu na sekta zote zikazorota. Watumishi wakawa hawataki kufanya kazi kule.

    Leo hii kumekuja neema ya gesi serikali bado inataka kuendeleza dhuluma zilezile kwa mikoa hii.

    Kiukweli niliposikia Prof. Muhongo ameteuliwa kuongoza wizara ya nishati na madini niliamini kuwa sasa wizara imepata kiongozi. Prof. Muhongo ni mwanataaluma aliyebobea kwenye masuala ya nishati. Nikadhani atafanya kazi kitaaluma zaidi na kuweka kando siasa. Lkn maajabu ni kuwa ameibuka kuwa mwanasiasa safi mno. Utaalamu wake wote umemezwa na siasa. Hoja alizozitoa hazifanani na uprofesa. Madini, mkonge, kahawa, pamba, nk. zinawanufaishaje moja kwa moja, mtu mmojammoja wa Mtwara na Lindi? Hakika ni aibu kwake kuendelea kutawaliwa na siasa namna hii. Nina hakika sasa ameshafikiria kwenda kugombea ubunge kule Tarime ili apige vema siasa.

    ReplyDelete
  3. Tatizo kwa mmoja ni opportunity kwa mwingine. Hiyo ndiyo siasa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. mbona inaonekana kuna ubaguzi? je wale wenye sehemu zenye utajiri wa dhahabu, inawapasa nao kudai kufaidika na rasilimali hiyo peke yao?

      Delete


  4. Sasa zitto kabwe badala ya kulilia kigoma kulivyo kubaya ana lilia mambo ya mtwara na lindi??

    kusafirisha gesi ni muhimu sana lakini vile vile watu wa mtwara wasi achwe kwenye mazingira ya sinto fahamu

    ReplyDelete
  5. Unafiki mkubwa, nilijua tu watu watatafutia umaarufu hapo. Jaribuni kuomba ushauri kwa wataalamu mjue logic za kuzalishia umeme DAR. Hata mkipeleka viwanda huko mtaona maandamano mengine ya "Wageni wanapendelewa ajira" kutokana na kiwango kidogo cha elimu. Hebu shughulikieni matatizo ya msingi ya wananchi acheni kutaka umaarufu kwa kutumia matatizo na ufahamu mdogo wa wananchi! I do not support any politician but I support Tanzania hivyo msinimisquote.

    ReplyDelete
  6. Ningependa sana bwana michuzi hawa wanasiasa kama zitto kabwe kabla hawajafungua midomo ningependa sana serikari ipeleke wabunge wa vyama vya siasa pande zote mbili kule somalia wajionehe wenyewe faida ya kuropoka ropoka ovyo bila ya ya kuangalia au kujua maana Ya Tanzania na neno amani naomba sana bwana michuzi nyinyi mko na haki ya kuelimisha jamii naomba serikari kwa kushirikiana na serikali ya Somalia na amisomu na uganda muende somalia ill hawa wanasiasa wajifunze kujenga siyo raisi lakini kubomoa ni dakika moja na sasa kama watu wenye akili finyu na nazikijinga wanaanza kuongea mambo ya kijinga basi maneno ya Baba wataifa yakitokea ndiyo mtajuwa maana ya amani mimi ni mtani wenu kutoka Uganda mtaenda njia ya somalia,
    mukasa

    ReplyDelete
  7. kweli akili ni zaidi ya kilakitu katika maisha haya.....ni akili tu ambayo wazungu kwa uchache wao waliitumia kuja afrika na kututawala woote kwa ujinga wetu....na ni kweli kama jirani yako ataendelea kuwa maskini kamwe hata uwe na mali vipi wewe uliyekaribu naye zaidi utakuwa maskini tuu wa kifikra

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...