Mwakilishi Mkazi wa Taasis ya Kimataifa inayojihusisha na kuwasaidia viziwi-wasioona nchini (SENSE INTERNATIONAL ) Christopher Andendekisye, akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari wakati wa mafunzo juu ya shida wanazozipata walemavu hao  na namna ya kukabiliana na tatizo hilo nchini sambamba na kujadili ukubwa wa tatizo pamoja na vyanzo vya matatizohayo.
Afisa wa Mipango (CBR Program Officer) wa Taasisi ya Kimataifa Inayojihusisha na kuwasaidia Viziwiwasioona Benjamin Kihwele, akitoa mafunzo kwa waandishi wa habari waliohudhuria mafunzo juu ya shida wanazozipata viziwi-wasioona na namna ya kukabiliana nan a tatizo hilo nchini sambamba na kujadili ukubwa wa tatizo.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mafunzo hayo ya siku moja leo jijini Dar es Salaam wakifuatilia kwa makini ili kuweza kuelewa vizuri mada zilizokuwa zikiwasilishwa kwenye semina hiyo.
Mwakilishi Mkazi wa Taasisi ya Kimataifa ya Sense (aliyekaa) akiwaonyesha Video Waandishi wahabari inayoonesha watoto viziwiwasioona na changamoto wanazokabiliana nazo kwenye maisha ya kila siku. Waandishi walishitushwa na changamoto zilizopo kwenye ulemavu wa aina hiyo na kuitaka serikali kugeuzia macho kwenye utoaji huduma kwenye eneo hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...