Baadhi ya wakazi wa mkoa wa Mtwara Mjini wakiwa kwenye maandamano makubwa waliyoyafanya kupinga gesi kusafirishwa kwenda Dar!
Wakazi hao wakiwa na mabango yao yenye jumbe mbalimbali kama uonavyo pichani.
Waandamanaji wakiwa wamekusanyika kwenye moja ya uwanja mjni Mtwara wakipinga gesi kusafirishwa kwenda jijini Dar!
Mmoja wa wakazi wa mji wa Mtwara mjini akiwa amebeba bango lake.
Baadhi ya askari wakiwa kwenye gari yao wakiangalia usalama wa hapa na pale kufuati maandamano makubwa yaliyofanywa na wakazi wa Mkoa wa Mtwara,wakipinga gesi kusafirishwa kwenda jijini Dar!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 30 mpaka sasa

  1. WAMAKONDE WANASHANGAZA,SIONI KWA NINI WAZUIE GESI KUJA DAR,NINA IMANI ITAANZIA KWAO HALAFU NDIO IJE DAR.SERIKALI IANGALIE KAMA KUNA MKONO WA WANASIASA.

    ReplyDelete
  2. Karibu nchi itagawanyika kimajimbo?

    ReplyDelete
  3. Hawa watani zangu Wamakonde wamenifurahisha sana. Kusema kweli wanachodai ni cha msingi. Hili tatizo hutokea sehemu nyingi duniani kwa mfano Nigeria ilifikia mpaka watu kushika silaha kwa sababu sehemu ambazo mafuta na gesi inakochimbuliwa kumesahauliwa kabisa kimaendeleo. Pia maandamano kama haya ni dalili nzuri kuwa Watanzania tumeanza kuamka.

    ReplyDelete
  4. We anonymous wa kwanza ndio MTUPU kabisa KICHWANI kama hujui basi maana yake ni kwmba UMEME uzalishwe Mtwara ili watu wapate ajira na sio kuuleta Dar
    Unakimbilia mkono wa KISIASA kweli wewe HAMNAZO

    ReplyDelete
  5. Sidhan wewe anonymous wakwanza unajua wenzio wanachokitaka fuatilia vizuri hilo si suala la umakonde Hoja ya msingi kwanini kiwanda cha kurefine (kusafisha) gas kijengwe DSM na sio mtwara inakotoka gas then isafirishwe refined gas kwenda sehemu mbalimbali. Kiuchumi inaimpact kubwa sana kwa watu wamtwara ikiwa hiyo itasarishwa kwenda kusafishwa DSM. Usikurupuke fuatilia vitu vizuri

    ReplyDelete
  6. ule umeme wa MW 18 wa Songas ulishindw kutumika Mtwara kwa sababu hawana uwezo wa kulipia sasa yule anayesema umeme uzlishiwe uko anajua usafirishaji wa umeme hupungua kutokana na umbali? Mtwara wanahitaji viwanda vya kazi kama vya saruji na mbolea pia bandari ili kunusuru hali yao ya maisha kwa kupata kazi huko kwa kuanzia zisizo za ujuzi mkubwa wakati vijana wakisomeshwa! Huu ndio ukweli kwa uchumi, rasilimali zile haziwezi ngoja mpaka Mtwara wanufaike kwanza! Mbona wao wamenufaika na Dar kipindi chocte wameuza vinyago vyao wamefanya kazi za ulinzi na sasa za Kimachinga? Hizi siasa za changu mimi changu bali chako changu zinatupeleka pabaya!

    ReplyDelete
  7. Wana haki ila sio kuizuia isiende Dar bali kushinikiza nao wapate hata kabla ya kwenda dar. Mbona madini yananufaiha nchi nzima wakati hayachimbwi nchi nzima?Mbona utalii wa Ngorongoro, Serengeti,Kilimanjaro n.k unanufaisha taifa zima na watu wa sehemu hizo hawajaandamana kupinga?

    ReplyDelete
  8. KUNA HOJA ZA MSINGI KWA WANANCHI WA MTWARA WANAHITAJI KUSIKILIZWA NA KUELEWESHWA VIZURI. VINGINEVYO TUNAALIKA VURUGU ZISIZO NA SABABU. ILA KWA UPANDE MWINGINE TUANGALIE BAADHI YA SABABU ZINAZOKWAMISHA MAENDELEO MTWARA. MATHALANI NA HAO WAWEKEZAJI WAKIJA MTWARA WATAKAA NYUMBA ZIPI? MBONA WAKURUGENZI NA MADIWANI WA MTWARA HALMASHAURI NA PIA MANISPAA WOTE KWA UMOJA WAMEKALIA VIWANJA VILIVYOPIMWA MIAKA 3 - 4 ILIYOPITA MSIJUTE NA MITENGO BILA KUVIGAWA, TENA HATA KWA MFUMO WA TENDA KWA KUTANGAZA NA KURUDISHA GHARAMA ZOTE ZA UPIMAJI. HILO TU LIMEWASHINDA WANALUMBANA MIAKA, JE TUTAFIKA? HEBU VIONGOZI WATUMIKIENI WANANCHI SI MATUMBO YENU NA AMKENI WAAMBIENI WATU UKWELI ILI VURUGU ZISIZO NA SABABU ZISIWEPO.

    ReplyDelete
  9. hawa wamakonde( ndugu zetu wa mtwara) nadhani nia yao na madai ni ya sahii ILA wanakosea kusema kuwa gesi isipelekwe DAR..ni upumbavu mkubwa wa kutokujua mambo ya dunia...mbona nyie wamakonde huwa hampigi kelele pale korosho zenu zinapopelekwa ulaya au DAR kuuzwa ? acheni upuuzi huo..biadhaa yenu ya hiyo gesi ni lazima ipelekwe sokoni kwa wateja ili ikauzwe na sokoni ni DAR..kama mngekuwa mnashindikiza viwanda vya ku-process hiyo gesi vijengwe mtwara hiyo ingekuwa hoja sahii..mnachokiongelea nyie wamakonde ni sawa na kumwambia mchaga kuwa kahawa yao yote isipelekwe sehemu nyingine yoyoye zaidi ya mkoa wao !! Amkeni nyie watu wa mtwara....bidhaa yoyote lazima ipelekwe waliko wateja na wanunuzi..mpoooo ?

    ReplyDelete
  10. Unapoona hoja zinazotumika ni UKWERE na UMAKONDE basi fahamu fika Tanzania si moja. Hii ni moja wapo ya alama za UKABILA, UMAJIMBO, UMKOA unaoimega vipande vipande Tanzania ya sasa. Tunayo kazi kubwa ya kurejesha UMOJA WETU, UDUGU WETU NA USAWA WETU KWA MASLAHI YETU KAMA TAIFA MOJA vinginevyo mambo si shwari huko mbele ya safari. Niger Delta ni mfano hai.

    Amani Millanga

    ReplyDelete
  11. mwambie huyo anaedai kuna siasa humo.kuna ulazima gani wa kuhangaika kuweka mabomba ya kusafirisha gesi hadi dar?.viwanda vijengwe hapohapo mtwara na malighafi isanifiwe palepale halafu sisi wa bagamoyo, dar, singida pemba na kwingineko tupate products zake tu.kina mtu afaidi kwa namna yake.

    wamakonde komaeni na hili hadi kieleweke. sio kila kitu dar, ndio maana foleni inaongezeka kila saa, eboooo!!

    ReplyDelete
  12. Big-up wamakonde kwa madai yenu ya msingi, lakini issue ya Bagamoyo inakujaje wakati umeme unakuja Dar?

    ReplyDelete
  13. watu wanaishi dar tu. Wakikaa na gesi yao wataweza kuinunua???

    ReplyDelete
  14. wanadai haki yao wanachotaka ni maendeleo kutokana na hiyo gesi.Sio kulundika kila kitu Dar.

    ReplyDelete
  15. Naungana na mtoa maoni wa 1. Watz wenzangu, tuamke, tusikubali kupelekwa pelekwa tu na wanasiasa bila sisi wenyewe kuchekecha jambo linaloletwa mbele yetu na kupima uzito wake. Kama sikosei imekuwa ikielezwa wazi kuwa gesi iliyokwishapatikana ni nyingi sana na inazidi kuvumbuliwa. Sasa enyi wamakonde uchoyo wa nini? Serikali imesema bayana hamtaachwa hivihivi, maendeleo yatokanayo na gesi hiyo yataanzia kwenu, ss tatizo lenu nini hasa? Cha ajabu zaidi hao wanaowashawishi kuandamana kupinga gesi isiletwe Dar es Salaam wameshindwa kuwashawishi katika masuala ya msingi kama vile kupiga kitabu kwa nguvu zote. Mfano mzuri ni hizi fursa zilizotolewa ili vijana wenu wasome masuala ya gesi asili na mafuta. Nafasi za kusoma bure zimetolewa kwa vijana wa Mtwara na Lindi, lakini hamjitokezi kuomba. Msaidiwe vipi? Kaaaazi kweli kweli.

    ReplyDelete
  16. Kiukweli maendeleo lazima yapatikane mikoa hiyo. Mbona serikali imewapelekea barabara ya lami na umeme sasa kuunganishiwa wa bei chee karibu na bure sasa sioni wanabweteka nini hawa watani zangu. Ajira pia watapata za kumwaga. Nigeria wao wana matatizo yao, hapa ni tz kisiwa cha amani

    ReplyDelete
  17. inabidi muangalie kiundani zaidi..before hamjaconlude,, je mtwara kuna mioundo mbinu ya kutumia gesi kwa sasa? je mtanyimwa hiyo gas mkishakuwa na miundo mbinu? je wanyimwe wenye miondombinu (dar) tayari, msubiriwe nyie? Je Dar sio Tanzania? umeshatafiti gharama ya kusafirisha ges from mtwara tu DAr ambapo tayari kuna mitambo ya umeme inayounganisha almost tanzania nzima na gharama ya kuunda mitambo mengine mtwara na kuweka grid ya taifa.. All in all sioni logic ya maandamano kama vile tayari mmenyimwa haki ya msingi. Kuhusu ajira mtapata as engineer wa mitambo , na hamjakatatwa kuomba ajira dar hata kama ww ni mtwara. Nadhani tunapoelekea si kuzuri kuwa na matabaka ya kiregion.

    ReplyDelete
  18. Ndiyo maana yu anonymous. Mpe gesi kabla hajatoa gesi pwaa!!

    ReplyDelete
  19. Jamani kuna anony hapo juu anadai madini yananufaisha nchi nzima. Labda yeye amenufaika. Mimi sijaona manufaa yoyote.

    ReplyDelete
  20. Kinachohitajika hapo ni Elimu. Kama kuna hata vijana wao waliosoma hata mpaka kidato cha nne tu wana uwezo wa kuwaelimisha kwa nini itakuwa haina tija kuzalisha umeme pale Mtwara na manufaa ya kitaifa yanapatikana zaidi umeme ukizalishiwa Dar. Inabidi mtu ajue kwwanza umeme unasafirishwaje na kuna gharama gani kuusafirisha, halafu alinganishe na gharama za kusafirisha gesi. Kitaalamu, kusafirisha gesi ni "efficient" zaidi au in tija zaidi kuliko kusafirisha umeme kwani umeme unaposafirishwa asilimia kubwa hupotea njiani. Hivyo kwa kuwa mahitaji ya umeme Mtwara ni madogo ni vizuri kuzalishia umeme Dar ambapo utaingia kwenye gridi ya Taifa na kupunguza upotevu. Ninachoweza kuwashauri jamaa zangu hapo Mtwara ni kutumia fursa ya upatikanaji wa umeme wa uhakika kugundua mambo ambayo wanaweza kufanya kwa ajili ya kuleta vipato. Sasa wanaweza kuanzisha viwanda vya saruji na chokaa ambavyo mwanzoni ilikuwa si rahisi kutokana na kutokuwa na umeme. Kuna mengi wanaweza kufanya na ni pale tu watakapoamua kutumia akili na kuyaona kwani fursa hazionekani kwa macho bali kwa akili. Hiki wanachofanya sasa ni kutokana na kuwa na uelewa mdogo pamoja na ushabiki wa kisiasa.| Lakini cha kuwshangaza ni kwamba ukifuatilia utakuta kuna watu wana degree na wamehusika na hayo maandamano na hawajajishtukia tu kwamba wamebugi men!

    ReplyDelete
  21. Na hawa wa kutoka Nchumbiji wache zaooo hizo3

    ReplyDelete
  22. Watu wanawashangaa Wamakonde kupinga gesi kupelekwa Dar. Wanasema eti mbona utalii unanufaisha nchi nzima. Hivi utalii unamnufaishaje moja kwa moja Mmakonde wa kule Mtawanya Mtwara? Watu hawajuwi kuwa utalii, madini, na kilimo katika ukanda wa kaskazini ndio ulioendeleza miji ya Arusha na Moshi? Utalii na madini ya kaskazini hayawezi kuathiri moja kwa moja maisha ya watu wa kawaida wa kusini au magharibi.

    Gesi ikichakatwa Mtwara, mzunguko wa pesa utaongezeka na kuvutia wageni wengi zaidi na kubadili maisha ya watu. Kutakuwa na ongezeko la shughuli za kiuchumi. Mikoa ya kusini haijaunganishwa ktk gridi ya taifa. Gesi ikichakatwa Mtwara na kuzalisha umeme mikoa ile itapata fursa ya kuunganishwa ktk gridi ya taifa. Miundombinu, ikiwemo barabara ya Kibiti-Lindi, Bandari, na Viwanja vya ndege vya Mtwara na Lindi itaimarishwa. Tukumbuke kuwa mikoa hii ndiyo inayozalisha korosho, zao la biashara linaloongoza kuiingizia taifa fedha za kigeni kwa sasa lkn viwanda havifanyi kazi, ukosefu wa umeme wa uhakika ikiwa ni moja ya sababu.

    Tujifunze sasa kugawa rasilimali. Kaskazini kumeshaendelea sana. Acha tupanue maendeleo sehemu nyingine za nchi. Mtwara ikiendelezwa kutapunguza wimbi la vijana kukimbilia Dar maana watapata fursa kulekule.

    ReplyDelete
  23. Hata Wasukuma dhahabu na almasi zao je vipi?

    ReplyDelete
  24. Blah blah blaaaah blaaah blaaah. Ujinga mtupu. Elimu duni, siasa mbovu na fikira potofu. Blaah blaaah blaaah. Mbunge kidato cha kuunga unga Mkonge, viongozi wengine vimeo sidhani hata kama shule wamemaliza. Blaaah blaah kama nafasi za jeshi na polisi zinazokuja Mtwara zinajazwa na watu kutoka sehemu nyingine mnatarajia mpate manufaa ya gesi? blaaah blaaah blaaah. Kama hata watu wa kujaza nafasi za Ulinzi kule Artumas walikosekana ajira gani mnazozungumzia? Kama korosho zinazowafanya muwe wazalishaji wa pili wa pato kubwa hazijawanufaisha. Blah blah blah bla. Acheni porojo. Jengeni Misingi. Somesheni watoto wenu, punguzeni idada ya ndoa na jengeni nyumba za tofali za kuchoma.

    ReplyDelete
  25. Nadhani ndugu zetu wa Mtwara wana hoja ya msingi. Umeme unazalishwa Kihansi na kusafirishwa hadi Dar. Kwanini usizalishwe Mtwara na kusafirishwa hadi Dar huku njiani ukimulika maeneo mengine anzia Tunduru, Songea, Mbinga, Ludewa nk.

    Bomba la gesi kwenda Dar ni muhimu kwa sababu ya watumiaji wa gesi viwandani. Lakini viwanda na mitambo ya kusafisha na kusindika hiyo gesi (LNG) vibaki Mtwara.

    Ni kweli miundombinu ya Mtwara ni duni na kila mwekezaji angependa ku-operate Dar. Lakini hapa ndipo nawashangaa TIC kwa kutoa incentive zinazofanana kwa nchi nzima. Waende Msumbiji kuona mfano. Kama incentive nzuri zaidi zikitolewa kwa mikoa ya pembezoni kama Mtwara, Lindi, Kigoma nk wawekezaji watakwenda huko.

    Kimaro

    ReplyDelete
  26. Bwana Blahblah umebobea kwenye blahblah! Huna hoja ya maana. Unadhani kwanini wananchi wale wanakumbana na matatizo uliyoyaorodhesha? Moja ni kupuuzwa na serikali. Mikoa ya kusini ilikuwa haifikiki kwa barabara hadi mwaka 2007. Hakukuwa na umeme hadi juzi baada ya gesi kuanza kuchimbwa. Wafanyakazi wa umma na binafsi walikuwa hawaendi kule. Shule hazikuwa na walimu. Wangeendeleaje? Kumbukeni ukandamizaji wa namna hii ulianza tangu ukoloni ambapp mikoa ile ilitengwa maalum kwa ajili ya kutoa nguvukazi ya kwenye mashamba ya mkonge/kahawa na kwenye migodi ya madini. Maendeleo mnayoyaona kwenye kanda zingine za nchi yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na watu wa kusini. Someni historia ili kujifunza. Acha kupiga blahblah!!!!

    ReplyDelete
  27. mbunge elimu ya kuungunga anasema muungano wa tanganyika na zimbabwe..........blahh blahh kweli mdau hapojuuuu

    ReplyDelete
  28. Blah blah oooh blaah blaah huna hoja akha umesema hoja au haja? blaaah blaaah Ndugu yangu; mimi blah blah nimeongea ukweli tu. Kama na wewe unaguswa pole sana. ila na wewe acha blah blah zako. Nafikiri si watu wote wa kusini walichukuliwa wakati wa ukoloni kwenda kwenda mashamba ya katani kama unavyodai. hizo ndiyo naziita blah blah blah Wala Wamakonde hawakupelekwa kagera au Moshi kulima kahawa! Hizo ni blah blah. wao walikuwa na mashamba yao ya karanga kule Nachingwea; unafahamu. Kule Farm 17. Ni kweli Wayao na Wamakonde kutoka Msumbiji walitumika kwenye manamba. Si Wamakonde wa Mtwara! Nani asiyewajua kwa uvivu? acha blah blah blah na wewe. Kuna mtu anaweza kumchukua kijana wa Mikindani akalime manamba? au Mmwamba wakati hata kushika jembe hajui? acha blah blah blah Mtwara ipi unayoizungumzia ambayo haikuwa na umeme? au unamaanisha matatizo ya jenereta? Mtwara ya Chikongola, Mtwara ya Majengo na Shangani imekuwa na umeme tangu mimi nimepata fahamu. Mtwara imekuwa na maji tangu nikiwa mdogo! Mtwara ya vijijini au? Ukiacha utendaji mbovu hata watu wa Newala na Mahuta walikuwa na Maji kutoka Makondeko! Ni Mtwara ipi unayoisemea wewe? Nafikiri kwa wazee wetu wengi elimu ya kizungu haikuwa suala la muhimu kiasi hicho ndugu yangu. Kama unaijua Mtwara basi utafahamu watu wa Maeneo kama Mnyambe, Mtopwa, Mkwedu, Chitangari na hizi sehemu zingine za Ndonde wamesoma. Umewahi kujiuliza kwa nini? acha historia za kuandikiwa na watu. Wewe ndiye usiwe na hoja hujatafakari kabla ya kuanza kunikosoa. Ninyi ndiyo mnaoishi vitabu. Hivi watu walio sawa wanaweza kuruhusu mtu mmoja kugombea majimbo matatu tofauti na kushinda? Ndiyo maana nasema na narudia hizi ni blah blah blah. Shida ya watu wa Mtwara ni kujaza matumbo yao tu. Ndiyo maana mtu anahamia Mtwara na mkewe miaka miwili mkewe anakuwa mbunge wa viti maalumu! Acha blah blah bla. Unajua kama watoto wenu hawajasoma hiyo gesi hata ikifanywa vipi haitowasaidia kamwe. Mnahitaji mipango na uratibu. Si maandamano. Korosho miaka na miaka imewanufaisha nini? Zile shule zenu za Mangamba, Masasi Girls na ndwika walipita humo wengi ni wageni. Walimu waliokuwa wanafundisha wengi wanatoka Ruvuma. Serikali ilikuwa inawakataza msisome?? Akina Mkapa, Lawi Nangwanda Sijaona, Musa Nnauye, Ana Abdallah, Nasoro Malocho walisomea wapi? Akina Namata walisomea wapi? Acha blah blah angalia kiini cha tatizo na nyie mkisoma kidogo tu mnakimbilia Dar. Mwisho narudia tena acheni blah blah blah.

    ReplyDelete
  29. Blahblah una kila sababu ya kujivunia blahblah maana ndio stahili yako. Ni umeme gani unaozungumzia Mtwara? Umeme uliokuwa unawaka saa 6 kwa siku tena hadi mafuta yawepo? Umeme ambao ulikuwa unaweza mupotea hadi mwezi mafuta yakiisha? Umeme wa kusini utafananisha ni wa gridi ya taifa? Maji gani unazungumzia? Maji ya Mkunya ambayo yakitoka ni sherehe? Na kwako wewe Mtwara ni Chikongola peke yake? Ni Newala gani yenye wavivu? Ushasikia wapi Newala wana njaa? Unadhani gesi ni ya Mtwara mjini? Farm 17 unayoisema inafanana na mashamba ya mkonge, kahawa, ngano, miwa, migodi lukuki ya kaskazini? Kumbuka mikoa ya kaskazini imeendelea kwa sababu ya kilimo cha kibiashara cha mashamba makubwa ya makampuni, si vishamba vidogovidogo vya wananchi. Nani kakwambia eti wamakonde hawakupelekwa manamba? Nenda Tanga kaulize. Wasomi wa mwanzo serikalini walitoka wapi? Biashara ya watumwa ya mwanzo ilifanyika wapi? Blahblah, kumbuka kuwa mambo haya yanajengana. Hali unayoiona leo inatokana jana. Jifunze historia kuwa miji ya mwanzo kuendelea Tanzania ni ya Kusini (Kilwa, Mafia, Lindi. Mikindani). Km wangekuwa wavivu wangepataje maendeleo? Nini kimebadilika leo hadi kuwe maskni? Jua kuwa ni mifumo ya utawala.

    Mtu umejifungia Chikongola afu unabwabwaja maneno wakati hujuwi lolote. Unasikia tu Arusha wameendelea ndo u adhani bure. Ni juhudi za serikali za kikoloni na huru ndizo zilizoleta tofauti. Utaendeleaje wakati barabara inayounganisha wilaya moja na nyingine haipitiki achilia mbali Kibiti Lindi.

    ReplyDelete
  30. Bwana Blanblah, nilisahau kujibu hoja yako nyingine ya ubunge. Unashangaa mtu mmoja kugombea majimbo tofauti na mushinda. Unaonesha ulivyo na akili za blahblah. Augustino Mrema amekuwa mbunge wa majimbo mangapi? Husein Mwinyi amekuwa mbunge wa majimbo mangapi? Makongoro Mahanga amekuwa mbunge wa majimbo mangapi? Stephen Wasira?. Unazungumzia mtu asiye wa kusini kupata ubunge. Soma kijana, orodha ni ndefu. Km huna taarifa uliza badala ya kubwabwaja pumba mbele za watu. Watu wanajadili mambo ya maana hapa wewe unaleta blahblah.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...