Octoba 1, 2012 NMB ilizindua promosheni ya Ki-COLLEGE zaidi na NMB inayowawezesha wanafunzi wenye akaunti ya NMB Student Account kupata nafasi ya kuingia kwenye droo na kujishindia zawadi mbalimbali kama: iPad, Samsung Galaxy, Amana maradufu, flash disk, fulana za NMB, taa inayotumia mionzi ya jua. Hivyo basi, wanafunzi waliofungua NMB Student Account, walioweka amana katika akaunti zao au kujiungana NMB mobile wameweza kuingia kwenye droo na wamepata nafasi ya kujishindia zawadi kwenye promosheni ya Ki COLLEGE zaidi na NMB.
Katika droo ya kwanza ya Ki COLLEGE zaidi na NMB iliyochezeshwa tarehe 12 Novemba, 2012, jumla ya washindi 66 walijishindia zawadi mbali mbali na katika droo hii ya pili washindi walijishindia Zawadi mbali mbali ikiwemo; Ipad 1, Samsung Galaxy 1, Amana maradufu 2, taa inayotumia mionzi ya jua 10, flash disk 50 na jezi za timu ya Taifa 10.
Mwanafunzi wa chuo Kikuu cha Mzumbe- Morogoro, Beatrice Chande akibonyeza kitufe kuwapata washindi wa promosheni ya Ki-College zaidi na NMB. Kutoka (kushoto) ni Meneja Masoko wa NMB, Shilla Senkoro na Mkaguzi wa bodi ya michezo ya kubahatisha ya Taifa, Abdallah Hemedy, Meneja huduma kwa wateja wa NMB tawi la Mwenge, Elizabeth Highness na Afisa bidhaa wa selcom, Everline Simpilu.
Pamoja na kampeni hii, wanafunzi watakaofungua NMB Student Account wataendelea kufurahia huduma za NMB Student Account kama: Kufungua akaunti kwa Sh. 10,000 tu (pamoja na NMB ATM kadi), kujiunga na huduma ya NMB mobile bure kupata huduma ya ujumbe mfupi kila utoapo fedha kwenye ATM ya NMB bure, kuchukua fedha hadi Sh.1,000,000 kwenye NMB ATM kwa siku na kupata huduma kupitia matawi zaidi ya 143 na NMB ATM zaidi ya 450 nchi nzima.
Ili uweze kuingia kwenye droo na kupata nafasi ya kujishindia zawadi kwenye promosheni ya Ki COLLEGE zaidi na NMB, fungua NMB Student Account, weka amana katika akaunti yako, tumia au jiunge na NMB mobile .Ikiwa hujatumia akaunti yako kawa muda mrefu tembelea tawi la NMB ili nawe ushiriki katika promosheni hii ya ki-COLLEGE zaidi na NMB inayoendelea hadi Desemba 31, 2012.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...