Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Jumuiya ya Watanzania, Mama Juliet Kiswaga akitoa neno la kuwakaribisha mabalozi, na wageni wengine waalikwa waliohudhuria hafla hyo iliyofanyika katika Ukumbi wa Kanisa la Holy Trinity Orthodox- New Rochelle.
Naibu Balozi Ramadhan Mwinyi akiwasalimia watanzania na kuwakumbusha wajibu wao wa kuiwakilisha nchi yao popote pale walipo, akasema kuwa wao kama mabalozi wamekuja kufanya kazi na kushirikiana na watanzania " tupo hapa kuujenga na kuimarisha umoja wetu na si kuanzisha umoja , tushirikiane na tufanya kazi kwa pamoja".
Balozi Tuvako Manongi akiwasalimia watanzania hawapo pichani, pamoja na kuhimiza umoja, upendo na maelewano miongoni mwao, Balozi aliwasisitizia watanzania hao umuhimu wa kujiunga na mpango ujulikano kama Faidika na WESTADI (Welfare Scheme for Tanzanians in Diaspora). Akasema kuwa mpango huo ambao unahusu masuala ya Bima ya Afya ni wenye manufaa na gharama nafuu kwao wenyewe na kwa familia zao ambazo wameziacha Tanzania. Aidha Balozi aliwaasa pia watanzania hao kujivunia utanzania wao na kwamba wakati wowote wajisikie kuwa huru kufika Ubalozini kwa kile alichosema ni ofisi yao na kwamba wao kama mabalozi na kama walivyoaswa na Rais Jakaya Kikwete wakati anawateua kwamba, pamoja na majukumu aliyowatuma lakini wanawajibika kuwatumikia pia watanzania wenzao huko ugenini.
Waziri Mkuu Mstaafu, Mzee John S. Malecela akiwasalimia watanzania , katika salamu zake, Waziri Mkuu Mstaafu aliwaeleza watanzania hao kwamba walikuwa na bahati ya kuwapata Balozi Manongi na Naibu wake, ambao aliwaelezea kama watu wenye upendo, uchapakazi, uadilifu na kuwataka basi wawape ushirikiano na upendo wao, huku akiwatakia mabalozi hao kila la khei katika kazi yao hiyo aliyoitaka kuwa ni ngumu ya kuiwakilisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, na bila ya kusahau kuwatumikia watanzania wenzao.
Mabalozi wakikata keki walizoandaliwa na watanzania.
Waziri Mkuu Mstaafu, Mzee Malecela akiteta jambo na Balozi wa Uganda katika Umoja wa Mataifa, hapa wanakumbusha enzi za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki kabla ya kuvunjika, walipowahi kufanya kazi pamoja, wakati huo Balozi huyo waUganda akiwa kijana mdogo, bado anazikumbuka busara na uchapakazi wa Mzee Malecela ambaye amemuelezea kama hazina ya aina yake.
ukafika wakati wa msonsi wa nguvu ulioandaliwa na akina mama wakitanzania, na vitumbua pia vilikuwapo.
Mabalozi wa kiwa na wajumbe wa Bodi ya Jumuiya ya Watanzania
Mabalozi katika picha na kundi jingine la watanzania.
Mabalozi katika picha ya pamoja na sehemu ya watanzania waliohudhuria hafla hiyo.
Mabalozi katika picha na kundi jingine la watanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...