Dar es Salaam, 3rd December, 2012 Wateja wa M-Pesa kuanza sasa wataanza kununua bidhaa ndani ya duka la Shoppers Plaza lililipo jijini Dar es Salaam, kwa kutumia huduma ya M-Pesa. Kuanzia leo, wateja wote watazawadiwa muda wamaongezi wa shilingi 1000 kama ofa pale watakapolipia huduma au kununua bidhaa kupitia M-Pesa. 

Washirika wa Vodacom wanaotoa huduma zao kwa njia ya M-Pesa nchi nzima kwasasa wanafikia 200 wakati baadhi yao wanatoa huduma zikiwemo Luku, Ving’amuzi vya TV,huduma zamaji, kodi, malipo ya bima, malipo ya pensheni,michango, ulipaji wa mikopo,tiketi za ndege,huduma hii mpya ya ununuzi wa bidhaa katika duka la Shoppers, ambalo litakuwa ni duka la kwanza Tanzania kwa huduma hii kufanyika. 

Kulingana na Maelezo ya Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom, Rene Meza (pichani),ofa itatolewa kwa huduma ya kwanza utakayo lipia kupitia M-Pesa kwa bidhaa utakayonunua.

 “Kama unanunua Luku mara tatu kwa mfano,utapata shilingi 1000 lakini kama utanunua Luku na DSTV utapata ofa ya muda wa bure wamaongezi kwa kila muamala utakaotumia. Tunajivunia wateja wetu na tuna kila sababu ya kufurahi kwa kuwapatia ofa hii kabambe,” anasema Meza. 

Katika kipindi cha miaka 4 iliyopita, M-Pesa imesaidia kuboresha maisha ya watu wengi,najuhudi za kuiboresha huduma hii zinaendelea. 

Kwasasa Vodacom imekwisha imarisha huduma zake karibu nchi nzima. Watejawa M-Pesa hutumia miamala ya takribani shilingi bilioni 35 kwa siku, hiyo nikutokana na jinsi huduma hii ilivyo salama na inavyokubalika nchi nzima.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...