Mhe. Mathias Chikawe (Mb), Waziri wa Katiba na Sheria leo amezindua shindano linalodhamiria kuboresha Mpango wa Uendeshaji wa Shughuli za Serikali kwa Uwazi. 

Shindano hilo linaendeshwa na TWAWEZA kama mchango wake katika kuendeleza Mpango wa Uendeshaji Shughuli kwa Uwazi. Shindano lililozinduliwa na Mhe Chikawe linalenga kuwapa fursa wananchi hasa wanafunzi na vijana kutoa maoni yao ya jinsi yakuboresha huduma za Afya, Maji na elimu. 

TWAWEZA itazipatia shule zenye wanafunzi watakaoshinda Komputa Mpakato kama zawadi. Mpango wa Uendeshaji Shughuli za Serikali kwa Uwazi ulizinduliwa Rasmi Tarehe 20 September 2010 huko New York na Tanzania ni kati ya nchi 58 ambazo zimejiunga na Mpango huu mpaka sasa. 

Lengo kuu la Mpango huu ni kuzifanya Serikali ziendeshe shughuli zake kwa Uwazi, kuongeza uwajibikaji, kupambana na rushwa, kuwawezesha wananchi na kuinua kiwango cha utawala bora. Tanzania imechagua sekta za Afya, Elimu na Maji kuwa sekta ambazo zitafanyiwa kazi kwenye mpango kazi wake wa OGP.
Mhe Chikawe akiwa pamoja na Bw. John Ulanga, Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation for Civil Society (wa kwanza kushoto) na Bw. Richard Mabala, Mkurugenzi wa Tamasha baada ya kuzindua vijitabu hivyo.

Mhe Chikawe pia amezindua vijitabu vilivyoandaliwa na TWAWEZA ikishirikiana na Tamasha vinavyoeleza changamoto mbalimbali katika sekta ya Afya, Elimu na Maji na ushirikishwaji wa wananchi kwenye kufanya maamuzi ya kimaendeleo. Jumla ya nakala Milioni Nne zinatarajia kusambazwa katika shule za msingi na Sekondari.
Mkurugenzi wa TWAWEZA Bw. Rakesh Rajani akiongea machache wakati wa uzinduzi huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...