ABIRIA
wanaosafiri kwenda mikoani na nchi jirani wamekwama katika Kituo cha
Mabasi Ubungo jijini Dar es Salaam, baada ya nauli kuendelea kupanda.
Imekuwa kawaida kwa wamiliki wa mabasi kupandisha nauli katika kipindi kama hiki cha kuelekea katika sherehe za Sikukuu ya Chrismasi na Mwaka mpya .
Kutokana
na kupanda kwa gharama hizo abiria wameirushia lawama Mamlaka ya
Usafirishaji wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), kushindwa kusimamia
tatizo hilo.
Ubungo kwa sasa kuna msongamano mkubwa sana wa abiria wakiwa wamekwama katika kituo hicho cha mabasi huku wakiwa hawajui cha kufanya,kutokana na kupanda kwa nauli hususani mabasi yaendayo Mikoa ya Kaskazini (Arusha, Tanga, Kilimanjaro).
Mabasi
yaendayo Arusha na Kilimanjaro nauli zimefikia kiasi cha Sh
30,000,kutokana na wingi wa watu wanaohitaji usafiri huo, huku magari ya
Tanga nayo yakipandisha nauli mpaka Sh 15,000, kutoka Sh12,000.
Mmoja
wa abiria Joseph Kihiyo alisema wamekuwa wakiamua kurudi nyumbani
kutokana na bei zinazotozwa katika mabasi hayo kwa kuwa haziendani na
bei za awali hivyo zimewakwamisha safari yao.
“Kila
wakala humu ndani ana bei yake, yaani kwenda hapo Korogwe ninaambiwa
nitoe Sh15,000 wakati awali nilikuwa nikitumia Sh12,000 tu, “alisema
Kihiyo.
Alieleza
kuwa kipindi hiki cha sikukuu hizo kumekuwa na tabia ya ulanguzi wa
tiketi kwa kuwa kila mtu anapewa tiketi kwa kiasi chake cha pesa
alichotoa. Abiria mwingine Mussa Said alilalamikia hali ya kusumbuliwa
katika masuala ya usafiri kwa kuwavuta vuta na hata muda wingine
kuwaibia wakati wakiwalazimisha kupanda kwenye mabasi hayo.
“Humu
ndani kuna tabia za ajabu sana unaweza ukawa unavutwa ukasema
unapokelewa vizuri kumbe wengine wamekuja kuiba,” alisema Said.
Katibu
Mkuu wa Chama cha Mawakala Ubungo (Cmmu), Hamisi Maneno alisema matukio
yanayotokea kila siku katika kituo hicho yanasababishwa na kutokuwa na
ushirikiano kati yao na wamiliki wa mabasi pamoja na Sumatra.
“Kama
kungekuwa na ushirikiano wa Sumatra na wamiliki wa mabasi kwa kukaa na
kutambua matatizo yanyotukabili, hili suala la ulanguzi wa tiketi
lingekuwa limekwisha, lakini hakuna ushirikiano wowote na ndiyo maana
mambo yanazidi kuwa mabaya,” alisema Maneno.
Maneno
alisema ni jambo la aibu kwa nchi kama Tanzania iliyofikisha miaka 51
ya Uhuru lakini bado ina ubabaishaji katika sekta ya usafirishaji wa
nchi kavu.
![]() |
hivi ndivyo ubao wa nauli za halali za mikoani uliopo nje ya stendi ya Ubungo unavyoonekana. |
Matatizo ya nchi ya dunia ya Tatu,nchi iliyoshindwa kutawalika.
ReplyDeleteHivi hiyo serikali haina sheria ya vitu vidogo kama hivi kuvifuatilia au mpaka raisi aingilie, my god inakera!!!!
ReplyDeleteMnapatia nini tabu kusafiri kwa mabasi huku nauli zikizidi kupanda juu kuelekea XMASS?
ReplyDeleteKwa nini msiende na ndege mpya ya bei rahisi ya FASTJET?