Wachezaji wa Zanzibar wakiwa wamembeba kipa wao, Mwadini Ally baada ya kupangua mkwaju mmoja wa penalti, na kuiwezesha timu hiyo kutinga Nusu Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge baada ya kuifunga Burundi kwa penalti 6-5 kwenye Uwanja wa Lugogo, mjini Kampala, Uganda jioni hii. Zanzibar sasa itacheza na mshindi kati ya Kenya na Malawi.

Na Mahmoud Zubeiry, Kampala
ZANZIBAR imeingia Nusu Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge baada ya kuifunga Burundi kwa penalti 6-5 kwenye Uwanja wa Lugogo, mjini Kampala, Uganda jioni hii kufuatia sare ya bila kufungana ndani ya dakika 90.
Kwa matokeo hayo, Zanzibar sasa itacheza na mshindi kati ya Kenya na Malawi katika Nusu Fainali.
Shujaa wa Zanzibar leo alikuwa ni Abdallah Othman aliyefunga penalti ya mwisho, baada ya kipa Mwadini Ally kupangua penalti ya Abdul Fiston wa Burundi.
Manahodha wa timu zote, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ wa Zanzibar na Suleiman Ndikumana wa Burundin walipoteza penalti zao leo.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...