Na Mwandishi Maalumu
Waamini na wapenzi wa Bukoba na Kagera wamefurahi sana kumpata Baba Askofu Desiderius Rwoma (pichani juu) kama askofu wa Jimbo la Bukoba kumrithi askofu Nestor Timanywa ambaye amestaafu kufuatana na sheria za kanisa.
Waamini na wapenzi wa Bukoba na Kagera wamefurahi sana kumpata Baba Askofu Desiderius Rwoma (pichani juu) kama askofu wa Jimbo la Bukoba kumrithi askofu Nestor Timanywa ambaye amestaafu kufuatana na sheria za kanisa.
Askofu Desiderius Rwoma alizaliwa mwaka 1947 katika parokia ya Rutabo, Kamachumu jimbo Katoliki la Bukoba. Parokia moja na Mwadhama Laurean Kardinali Rugambwa. Alipata upadrisho kwa mikono ya Baba Askofu Nestor Timaywa, mwaka 1974 pale Rutabo.
· Akiwa jimboni Bukoba aliwahi kuwa gambera (Mkuu wa shule) ya seminari ya Rubya kwa miaka mingi. Wakati wake shule ya Rubya mara kadhaa ilikuwa ya kwanza kitaifa katika mitihani na karibu mara zote ilikuwa kila mara kati ya shule 10 bora taifani. Mapadre wengi vijana jimboni Bukoba walipitia mikono yake hivyo anawajua vizuri na wanampenda.
· Vile vile alikuwa mlezi wa kiroho wa shirika la masista wa Mtakatifu Terezia wa Mtoto Yesu, shirika la jimbo na hivyo analifahamu vizuri na kila mara amekuwa karibu nao.
· Kabla ya kuteuliwa kuwa askofu wa Singida alikuwa makamu wa askofu wa Bukoba na hivyo kulijua jimbo la Bukoba na uongozi wake. Alifanya kazi hii vizuri sana na hivyo kuteuliwa kuwa askofu wa Singida.
· Akiwa askofu wa Singida (1999 – 2013) ameonyesha karama zake za uongozi. Ameweza kuleta maendeleo ya kichungaji na kibinadamu katika jimbo. Ameonnyesha uelewano wake kwa kuwaalika mashirika mengi ya kitawa ambayo kila moja limeleta karama yake ya maendeleo, uchungaji, shule, vituo vya afya, maendeleo ya akina mama na vijana nk.
· Katika Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania anasimamia idara kubwa ya Utume wa Walei
Askofu Desiderius Rwoma ni mpole, mnyenyekevu, msikivu, muwazi na mpenda maendeleo. Ana uhusinao mzuri na kila mtu bila kujali hali, jinsia, kabila, taifa au dini.
WANABUKOBA NA WANAKAGERA WANAKUKARIBISHA KWA FURAHA NA SHANGWE, KARIBU NYUMBANI
Bishop D. Rwoma na Bishop Nestor Timanywa katika basi na mabishop wengine
Bishop Rwoma akiwa na baadhi ya Mabishop wazawa wa Bukoba
Bishop Rwoma na Bishop Dallu wa Geita
Bishop Rwoma na Bishop Kilaini wakiwa Singida
Bishop Rwoma akiwa na waseminari wa Singida
Bishop Rwoma baada ya kumuweka wakfu mchungaji mpya Singida
Oh! hongera sana Baba Askofu Rwoma, tunakuombea Mungu wetu akuongezee nguvu ya kuchunga kondoo wake.....Sijakuona miaka mingi tangu 1975 ulipokuwa pale Rubya ukiwa kijana, na sasa bado una nguvu zote ........Mungu wetu akijalie.
ReplyDeleteHONGERA SANA Baba Askofu. MUNGU MWENYEZI akubariki uongoze kondoo wake vizuri
ReplyDeleteAnkali, Aksante sana kwa taarifa ila ili kukienzi kiswahili basi tutumie ASKOFU badala ya BISHOP. Hii itasaidia sana.
Hongera sana Baba Askofu Rwoma. Naomba kuuliza, hivi askofu Kilaini anaendelea tu kuwa askofu msaidizi? Yeye hana sifa za kuwa askofu mkuu? Mwenye kujua hili naomba anijulishe.
ReplyDelete...I miss Bishop Kilaini, where is he now this distinguished man of God?
ReplyDeleteMimi nakumbuka ulipokuwa kocha wa timu ya mpira wamiguu ya Rubya ilikuwa inatisha kama njaa miaka hiyo ya 90!.Vijana wako walikuwa na uwezo wa kuzichemsha timu za ligi kuu wakiwa ndani ya uzi safi utafikiri ni the Gunners!
ReplyDeleteHongera Baba Askofu kwa uteuzi wako uliotukuka MUNGU akulinde akupe nguvu na uchape kazi ,kama ulivyokuwa jimbo la singida
ReplyDeleteMungu wa rehema akujalie mapaji yake saba katika kuchunga kondoo wake huku jimboni Bukoba
ReplyDelete