Wahandisi wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) wakikamilisha kufunga kioo kipya ambacho kimenunuliwa kutoka nchini Marekani cha ndege yao aina ya Dash-8 Q300 yenye namba za usajili SH-MWF ambayo ilipata ufa (Wind shield crack) tarehe 11 Januari, 2013, muda mfupi baada ya ndege hiyo kuruka kutoka Kigoma kurudi Dar Es Salaam katika safari zake za kawaida. 

Matengenezo hayo yanafanyika katika uwanja wa ndege wa Kigoma yakisimamiwa na Mhandisi Righton Mwakipesile na Mhandisi Merkior Karwani.

Uongozi wa ATCL umedhibitisha kuwa safari za Dar-Kigoma-Dar zitaendelea kama ratiba yao inavyoonyesha punde kuanzia kesho tarehe 22/1/2013. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Kila la kheri katika azma yenu ya kuwatumikia Watanzania!

    ReplyDelete
  2. Nina wasi wasi na utaalamu wa hawa mafundi. tezama wasivyo makini!

    ReplyDelete
  3. Bora na sisi na ATCL yetu tujikakamue hivyo hivyo kama mnavyoona Mwingereza Mtawala watu Mkoloni anafunga virago na British Airways yake mwezi March baada ya huduma za umri wa babu na bibi za miaka 82 nchini!

    Ama kweli nguo ya kuazima haisitiri makalio!!!

    ReplyDelete
  4. Seikali inabidi kujitoka kwenye masuala ya kibiashara. Piga mnada hili shirika kwa watu binafsi au mtaendelea kupata hasara kama kawaida. No profit motive.

    ReplyDelete
  5. kioo kimetoka marekani hahahaha ndio kutuonyesha kuwa ni kioo madhubuti chenye uhakika au vipi? mpaka tutajiwe kimetoka marekani ama kweli tutabakia kuwa watumwa mpaka dunia itaisha

    ReplyDelete
  6. sasa mbona hatuelewani hichi kioo kuna mdau alitufahamisha kuwa kimenunuliwa pale gerezani daresalaam sasa tunaambiwa kimetoka marekani mimi nasubiri iruke kama ikifika salama huko iendako tena ndio na mimi nitapanda sina uoga bali nachukua tahadhari ya lazima.

    ReplyDelete
  7. Mdau wa sita anony wa Tue Jan 22, 05:55:00 pm 2013

    ...sasa mbona hatuelewi hichi kioo kuna mdau alitufahamisha kuwa kimenunuliwa pale gerezani daressalaam...

    Hahahaha, ule Mnada ni funiko bovu, mimi nilishuhudia MAGURUDUMU YA NDEGE, SPEA ZA MELI na SPEA ZA VIWANDA pale vikiwa vimewekwa ubaoni kuuzwa!

    ReplyDelete
  8. BONGO KILA KITU KINAWEZEKANA!!!

    Ama kweli Bongo ndio maana wamesema tambarale!

    Nchi zingine maintenance za Ndege zinafanywa kwenye Hungers tena sio manmade hands ni kwa njia ya specific ROBOTIC AUTOMATION, tena zenye LDT (Leakages Detecting Technologies) ambazo hufunga screws za bodi ya ndege hadi fittings za matengenezo mengine!

    Ni kuwa nguvu ya mkono wa binaadamu haina pressing force kuweza kuhakikisha ya kuwa waki fix kioo hakutakuwa na leakeges (mianya) kwa vile Space (anga) lina physical forces (nguvu za upepo) ambapo kuna pressure(mgandamizo) pia ni mkubwa.

    Hapo kutokana na kuwa NISHANI YA NOBEL ILIYOTUKUKA DAIMA IPO TANZANIA, ni kuwa huyo fundi nguvu anayoitumia ni ya kushiba Chai ya rangi kwa chapati mbili na bakuli la maharage na sio ROBOTIC PRESSING FORCE kufunga screws za dirisha la ndege.

    Huko Ujerumani na Ufaransa haiwezekani na huwezi kushuhudia Wolkswagen (made in Germany) ikawekwa injini ya Peugeout (made in France),lakini Tanzania inawezekana ,mimi nilishuhudia Volkswagen Combi huko Tanga mwaka 1981 ikiwa na engine ya Peugeot 504 na rejeta pia.

    OHOOO,

    KILA KITU TANZANIA KINAWEZEKANA!

    ReplyDelete
  9. Hii wakiona Norway Kamati ya Nishani ya NOBEL itatutoa Kimasomaso Tanzania kushinda Tekinolojia ya mikono!.

    Kwa ufundi huu wa kuziba Kioo cha Ndege kwa kupanda juu ya Stuli na kwa mikono muda sio mrefu Mtanzania atamzidi Mchina HWANG-HO kwa kuunda Nyungo,Mitungi ya Maji,Vinu na Michi vyenye Redio na vyene ye kucheka!!!

    Tutashuhudia Nyungo, Mitungi ya maji na vinu vikiwa na Spika na ''answering machine'' za kuacha ujumbe wa Sauti endapo utamkuta mtu hayupo nyumani ameenda Kisimani kuchota maji au Shambani!

    ReplyDelete
  10. ATCL:

    Jamani isiwe tabu tukubali yaishe, Matengenezo ya ndege kwa mikono tena nje, sio ndani ya Hungers na kwa Robotics?

    Bora tuiuze ATCL na kugawa fedha za Mauzo kwa Waganga wa Kienyeji nchini kama Ruzuku ili waendeleze kutoa huduma za Usafiri wa Anga.

    Kwa nini tusiimarishe ile Idara yetu ya Kiasili (KURUKA NA UNGO) kama Idara ya Kisayansi ya kawaida (ATCL) tumeshindwa?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...