KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimkaribisha Balozi wa Uingereza hapa nchini, Diane Corner aliyemtembelea leo, Januari 22, 2013, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. kwa ajili ya mazungumzo maalum ya kikazi.
KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na mgeni wake, Balozi wa Uingereza hapa nchini, Diane Corner, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo Januari 22, 2013. Kushoto ni Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro na kulia ni Mkuu wa Mawasiliano na Siasa wa Ubalozi huo, Mark Polatajko.
KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiagana na Balozi wa Uingereza hapa nchini, Diane Corner, baada ya mazungumzo yao, leo, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo Januari 22, 2013. Wapili kulia ni Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro na kulia ni Mkuu wa Mawasiliano na Siasa wa Ubalozi huo, Mark Polatajko. (Picha na Bashir Nkoromo).
Michuzi nipo chini ya miguu yako naomba usiibane hii.
ReplyDeleteDk Asha Rose Migiro nakufagilia sana toka ulipokuwa UN..kwa kweli ulinifanya niheshimike sana mbele ya marafiki zangu huku ughaibuni kwa kukutaja wewe as mfano wa mafanikio ya uwezo wa m-tz.
Sasa dokta hiyo picha hapo juu unaonekana unachukua sijui minutes za kikao naona si sahihi kabisa.
Dokta bado unaheshimika sana kwa kushika position ya juu sana kimataifa so watu kama hao mabalozi wao ndio wanatakiwa kuchukua minutes za unachoongea.
Nadhani hiyo position kwenye siasa ni ndogo sana dokta inakushusha heshima na inatushusha heshima sisi tunaokupenda. Ingekuwa upo kwenye NGO ningeelewa unajitolea.
Plz dokta bora hata ukafundishe kuliko hiyo ya kupokea wageni&minutes.
Mdau
Finland
Da! Mdau Ufini maoni yako yanafanana. Na hata pose la hao wengine pichani nadhani ni la kama kumshangaa!
ReplyDeleteNaibu katinu Mkuu UN asichukue minutes hata kama amestaaf.
jb
Nakubaliana na na wewe hapo juu.mama anaheshima kubwa sasa nadhani hajui kama anaheshimika kama tunavyojua sie.maaana anaonekana anawanyenyekea wageni wakati yeye yupo juu kustaafu hakujakushuhia heshima yako mama,na lingine kama vipi rudi shuleni kafundishe siasa achana nazo ipo siku watoto wadogo wasio jua thamani yako watakuporomoshea heshima majukwaani.kwani vijana wengi wasio na ajira wanahasira na serikali hii .
ReplyDeleteMbona picha iko vizuri tu na haioneshi kama anaandika minutes. Hiyo ni tafsirir yako tu, mimi naona anaangalia points alizoandaa ili aweze kuwa makini na anachokiongea. Watu makini hawakurupuki, wanaongea kile walichopanga kuongea. Nadhani Watanzania tuache majigambo na kujikweza kusikokuwa na msingi tufanye na kushauri mambo yatakayoisaidia nchi yetu.
ReplyDeleteEddy
Van-ughaibuni.
mdau wa finland,nashukuru kwa maoni yako mazuri sana na kweli dr Migiro anaheshimika sana na amefanya kazi nzuri sana UN nakubali.ila japokua uko Finland ila bado mawazo yako ni kama bado ulipokua bongo enzi zile.
ReplyDeletekwanini nasema hivyo, kwanza mama Migiro ni msomi ambae amebahatika pia kuishi nje ya nchi yetu kwa vipindi tofauti,pili ni kiongozi mara nyingi viongozi wa kweli huwa hawajikwezi kwa madaraka au kwa kujikuza kama mungu watu.
ukiwa kiongozi lazma ukubali kupanda na kushuka,pia viongozi ni watumishi wajamii kwahiyo mama anaelewa hilo na kwa kufanya kazi kama wajibu ni sehemu ya maisha ya kila siku ya watu ktk jamii bila kujali ulikua na madaraka gani kabla ya (day job)yako.
namfananisha naibu katibu mkuu wa UN zamani na balozi Mwanaidi Maajar amabae anamaliza muda wake wa kulitumikia taifa letu nchi marekani na alikua Uk kabla,lakini anarudi nyumbani katika sekta binafsi.Hii ni mifano ya hawa akina mama wawili wanaoonyesha mfano katika nchi yetu na wanastahili kuigwa.
mfano marekani,ALGORE alikua (VP)KTK KIPINDI CHA bill Clinton akiwa kijana,muda ulipoisha na alipokosa uraisi baada ya kushindana na George Bush amerudi ktk maisha ya kawaida,na kwakua hakua na (any security risk)anaendesha SMART CAR mwenyewe.
kwahiyo watanzania tuyaangalie maisha na madaraka ktkt sura nyingine,na tujue hata bila ya madaraka maisha yanajengwa kilasiku katika hali ya kawaida na ndio maendeleo yatapatikana.
mdau washington.
Akichukua minutes kuna ubaya gani, pengine yeye ndiye alichaguliwa kuwa katibu wa kikao.
ReplyDeleteMdau wa kwanza ulichoongea ni kweli . Hata mimi nimeshtuka kuona Dr anachukua minutes.
ReplyDelete