MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), imetangaza bei kikomo cha bidhaa za mafuta kinachoonyesha kuwa petroli, dizeli na mafuta ya taa zimeshuka kuanzia leo. 

Taarifa iliyotolewa jana na Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Haruna Masebu imesema bei hizo zimepungua ikilinganishwa na toleo lililopita la Desemba 5, mwaka jana.

 “Katika toleo hili, bei za rejareja kwa petroli, dizeli na mafuta ya taa, zimepungua kwa viwango vifuatavyo: petroli Sh126 kwa lita sawa na asilimia 5.96; dizeli Sh32 kwa lita sawa na asilimia 1.60 na mafuta ya taa Sh50.74 kwa lita sawa na asilimia 2.50,” imeeleza taarifa hiyo. 

Kwa punguzo hilo, bei ya rejareja ya petroli katika jiji la Dar es Salaam itauzwa kwa Sh1,993, dizeli Sh1,967 na mafuta ya taa Sh1,973. 

Arusha petroli ni Sh2,077, dizeli Sh2,051 na mafuta ya taa Sh2,057. Katika jiji la Mbeya petroli itauzwa kwa Sh2,099, dizeli Sh2,074 na mafuta ya taa Sh2,079 na jijini Mwanza, petroli itauzwa kwa Sh2,142, dizeli Sh2,117 na mafuta ya taa Sh2,122. 

Taarifa imefafanua kuwa mbali na kupungua bei hiyo katika uuzaji wa rejareja, bei pia imepungua kwa katika uuzaji wa jumla ikilinganishwa na matoleo mawili yaliyopita. “Bei za jumla kwa kulinganisha matoleo haya mawili zimepungua kama ifuatavyo: petroli kwa Sh126.10 kwa lita sawa na asilimia 6.17; dizeli kwa Sh32.48 kwa lita sawa na asilimia 1.69 na mafuta ya taa kwa Sh50.74 kwa lita sawa na asilimia 2.6,” alisema. 

Mkurugenzi huyo amesema katika taarifa hiyo kuwa mabadiliko hayo ya bei, yametokana na kupungua kwa bei ya mafuta katika soko la dunia na kuimarika kidogo kwa thamani ya Shilingi ya Tanzania dhidi ya Dola ya Marekani.

 Alisema kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta ya mwaka 2008, bei za bidhaa za mafuta ya petroli, zitaendelea kupangwa na soko. “Ewura itaendelea kuhamasisha ushindani kwa kutoa taarifa za bei kikomo za bidhaa za mafuta. 

Taarifa hizi zina lengo la kuwasaidia wadau kufanya uamuzi stahiki kuhusu ununuzi wa bidhaa za mafuta,” alisema Masebu.

 Hata hivyo, Masebu alisema pamoja na mpango huo wa Ewura kuweka bei ya kikomo, kampuni za mafuta ziko huru kuuza bidhaa hizo kwa bei ya ushindani, ilimradi ziwe chini ya bei hiyo kikomo. 

Alivitaka vituo vya mafuta kuchapisha bei hizo mpya katika mabango yanayoonekana bayana na kuonyesha bei ya mafuta, punguzo, vivutio vya biashara au promosheni zinazotolewa na kituo husika. 

“Pale ambapo inawezekana kuchagua, wateja wanashauriwa kununua bidhaa za mafuta kutoka kwenye vituo vinavyouza mafuta kwa bei ndogo zaidi ili kushamirisha ushindani. Ni kosa kuuza mafuta bila kuweka mabango ya bei inayoonekana vizuri kwa wateja na adhabu itatolewa kwa kituo husika,” alisema. 

Masebu aliwashauri wanunuzi kuchukua stakabadhi ya malipo inayoonyesha jina la kituo, tarehe, aina ya mafuta yaliyonunuliwa na bei kwa lita ili itumike baadaye kama kidhibiti endapo kutajitokeza malalamiko ya ama kuuziwa mafuta kwa bei ya juu kuliko ya kikomo au yenye kiwango cha ubora kisichofaa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. I totally confused, why is oil still regulated by the Government. For sure the private sector could do better. Poor simple economics let demand and supply forces do their job Ndugu Masebu. They don't regulate cars, clothing, food and even education. Is oil not just another commodity?

    ReplyDelete
  2. Huu ni mchezo wa kuigiza!Watanzania lazima Wazinduke Sasa!Bei yoyote ya Petroli na Dizeli itakayo zidi shilingi 1,500/= kwa Lita Moja,bado iko juu sana,tena sana!Huu mchezo wa kupunguza shs.40/= au shs.60/= kwa Lita kila wiki au wiki mbili,na kufuatiwa na matangazo kibao,ni kuwageuza Watanzania kama vile akili zao hazifanyi kazi sijui? Be serious,maaann!Katika nyakati hizi za mitandao,watanzania kila kukicha,wanajua bei ya petroli nchini Marekani ni kiasi gani,bei katika nchi za majirani etu,Kenya,Uganda,Rwanda,Burundi,Zambia,Malawi,Congo DRC,etc.,nchi za Afrika Kaskazini na kwingineko,zikoje!Kwa hiyo SUMATRA waache kututania!If they cant regulate prices of petrol and other fuels to their realistic levels,they had better shut-up!

    ReplyDelete
  3. Anonymous wa hapo juu wacha kulisha watu uongo, kwanza unapaswa kujua kwamba EWURA "haipangi" bei ya mafuta bali inatangaza bei baada ya kuweka variable inputs (kama vile bei ya mafuta kama yalivyonunuliwa huko yanakotoka, freight charges, insurance na exchange rates)pamoja na fixed inputs kama kodi na tozo mbalimbali pamoja na margins za makampuni... Sasa unapodai kwamba bei haipaswi kuzidi shs 1500 kwa lita sijui unatumia kigezo kipi, na nina mashaka kama hata biashara ya mafuta waifahamu. Na pia usiwe muongo kudai kwamba bei ya mafuta Kenya, Uganda na Rwanda iko chini kuliko hapa kwetu. Kama ungekuwa mkweli basi ungetaja hizo bei za Rwanda, Kenya na Uganda. Na pia ni kichekesho kulinganisha bei ya mafuta Tanzania na ile ya Marekani na Afrika Kaskazini... Na sijui unaposema Afrika Kaskazini unamaanisha Libya na Algeria? Kama unamanisha nchi hizo basi ni dhahiri kwamba hujui lolote kuhusu sekta ya mafuta! Libya na Algeria zinazalisha mafuta zenyewe, na kama unamaanisha Egypt, ulipaswa kuzingatia ukweli kwamba location wise, Egypt iko jirani na nchi zinazozalisha mafuta kwa hiyo freigh charges zinakuwa chini!...

    ReplyDelete
  4. hebu weka hapa mjengoni breakdown ya bei ya lita moja ya petroli tuone mgawo wake umekaaje?kwanini mgeuze watu kama hawana akili?fuel is a basic input/necessity katika uzalishaji mali na usafirishaji wa bidhaa!kwanini wazalishaji wabebeshwe mzigo usio na tija?kwahiyo,ewura inalipwa kwa kutangaza tu bei kwa walaji,na sio kuwalinda?whats the use of having you around if you can not help bring down costs?chunguza kwanza,management structure ya ewura yenyewe,how costly is it?kuna madarekta na mameneja wangapi?na utitiri chungu nzima,nani anayebeba mzigo huo?kodi za aina ngapi zimefichwa ndani ya bei ya petroli?kwanini,bei ya dizeli ilingane na bei ya petroli?kwanini bei ya mafuta ya taa isiwe chini ya shs.800/=kwa lita?do you have those answers?acheni kuchekesha watu!uliza bei ya petroli Rwanda na Burundi,ikoje,linganisha na tya kwetu,na zote zinapitia bandari yetu ya Dsm,ungetegemea wao,plus transportation,bei yao ingekuwa hata mara tatu zaidi?check your factfile economisht wa ewura!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...