Mvua kubwa iliyonyesha mapema leo mjini Mtwara imepelekea mafuriko katika maeneo mbali mbali ya mji huu na kufanya wakazi wa maeneo haya kupata kuanza kuhangaika kuhamisha vitu vyao na wengine wakiwa hawajui la kufanya maana maji yamejaa mpaka majumbani mwao.Ni balaa kubwa la mafuriko ya maji Mtwara leo hasa eneo la Chuno. Eneo hili ni karibu na nyumba ya Mzee Hokororo au Dr Mwakipa. Hali ni mbaya sana na maji yanaendelea kujaa hadi mchana huu.Hakuna taarifa yeyote mtu yeyote aliyepoteza maisha. Msaada wa haraka unahitajika kwa wananchi hawa.Picha na Mdau Abdulaziz Video wa Globu ya Jamii,Mtwara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. oooh mafuriko ni moja ya rasilimali zao wana mtwara tusiwaingilie!

    ReplyDelete
  2. Mkwere ameanza uchawi wake sasa. Hamtapona na gesi yenu...

    ReplyDelete
  3. Watavuna wlichopanda. Dar hakuna msaada, wauze gesi.

    ReplyDelete
  4. Mafuriko ni mambo ya hali ya hewa tu, semeni yote lakini atimize kwanza madai yetu hata sisi uchawi tunao hatujali!

    ReplyDelete
  5. Serikali isiingilie wananchi wa mtwara na rasilimali yao ya mafuriko!

    ReplyDelete
  6. Ayaaa kumbe kuna mafuriko pia? nilijua gesi pekee

    ReplyDelete
  7. gesi ikisafirishwa kwenda dar itageuzwa maji, labda ndo maji yenyewe hayo yanasubiri bomba lilazwe from mtwara

    ReplyDelete
  8. Adhabu ni hapa hapa dadek!

    ReplyDelete
  9. Ni majibu ya Mwenyezi kwa watu wa MTWARA kudai gesi yote ni ya kwenu wakati imetafutwa kwa Mabilioni Fedha ya mali za wakazi wa Mikoa mingine nchini!

    Kwanza kiasi kikubwa cha gesi 74.9% ipo baharini sio katika Mkoa wa Mtwara ninyi mna 14.3% tu!

    Hivyo hayo mafuriko ni majibu ya Mwenyezi kwenu watu wa Mtwara kutaka kuwazika mali Watanzania wenzenu!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...