Meneja Mahusiano wa Multichoice Tanzania Barbara Kambogi (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya Mkurugenzi wa MultiChoice Africa kwa ukanda wa Afrika Mashariki Stephen Isaboke ambapo amesema Wateja wa huduma za Dstv nchini Tanzania wametakiwa kutokuwa na hofu ya kupata muingiliano au kukatika kwa picha katika kipindi hichi cha kutoka analogia kwenda digitali.

Barbara Kambogi amesema watanzania ambao wamejiunga na Dstv hawatahitaji kuhama kwa kuwa Dstv iko katika mfumo wa digital tangu awali.

Ameoneza kuwa Dstv imekuwa ikitoa huduma za digital televisheni kwa Tanzania kwa kipindi cha miaka 17 iliyopita, ambapo wateja wake wameweza kupata channel nyingi zaidi za kuchagua zikiwa na picha safi na sauti bora.

Kupitia vifurushi tofauti vinavyotolewa na Dstv wateja wanakuwa na maamuzi ya kuchagua kifurushi anachotaka na bei ambapo Ofa ya msimu wa Sikukuu za Krismas inaendelea pamoja na punguzo la asilimia 10 la kufanya malipo kabla ya muda uliolipia huduma kumalizika. Kulia ni Operation Manager wa Multichoice Tanzania Bw. Ronald Baraka Shelukindo.
Managa Uendeshaji wa Multichoice Tanzania Ronald Baraka Shelukindo akifafanua jambo kuhusu Televisheni nyingine kuingizwa katika huduma za DStv na kusema suala hilo litategemeana na makubaliano na mikataba na wamiliki pamoja na kutegemea uwezo wa Satelite.

Kwa Tanzania DStv inamkataba na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) la kuichukua TBC katika DStv Platform ambapo itakuwa inaonekana bure hata kama hujalipia king'amuzi chako chaneli hiyo haikatwi.

Bw. Shelukindo amewataka Watanzania kuendelea kununua ving'amuzi vya DStv kabla ya kuisha kwa Ofa ya msimu wa Sikukuu za Krismas na Mwaka mpya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Bwana kama hamko tayari kuturushia wakina ITV and the rest....TUTAHAMA!

    ReplyDelete
  2. dstv hawatendi haki hata kidogo yaani hawezi hata kuonyesha mbuga za wanyama wa tanzania tunaona manyoka na mamba sijui toka nchi gani na hiyo TBC bado haionekani kabisa pamoja na kutuhakikishia kuwa ni bure tunaomba sana waongee na watekeleze kw vitendo maneno yako

    DSTV maana yake mpira tu ndio imani ya watu wa TZ walio wengi this is not right at all.


    kwa nini tuone BBC na sio TBC

    ReplyDelete
  3. jamani hawa watu wanatupotosha. tuliambia kuhamia digitali chanel zote wanaziita local zitaoneka.
    Leo inakuwaje wanasema itategemeana na makubaliano na wamiliki
    Bila kujijua tunanunua haki ya kupata habariza nchi yetu wenyewe.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...