Ahsante kaka kwa uwanja huu wa kutoa maoni.
 
Mdau aliyeandika kuhusu kigamboni amenifanya niandike hili pia. Ahsante mdau kuliona hilo.

Ukizungumzia 'beach boys' sio kigamboni peke yake, daraja la Selander sasa limekuwa hatari. Hao vijana wanajificha baharini, pande zote za daraja, wakiona upenyo kidogo tu wanakuja kwa kasi ya ajabu na kupora kwenye gari, iwe ni sight mirror au chochote wanachoweza kukifikia. 

Hii ni hatari sana, kwani inaweza hata kusababisha ajali mbali ya madhara atakayokuwa ameyapata aliyeporwa. Haya yote yanafanyika mapema tu, na limekuwa ni jambo la kawaida kila siku giza likianza tu.
 
Swali la kujiuliza, wale askari waliokuwa wakilinda maeneo hayo wakisaidiwa na mbwa, wameenda wapi? Wadau tusaidiane katika hili, hali imekuwa mbaya.


Mdau Mwenge

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. Asante mdau pia sio hapo tu na mataa ya kwenda kekooo na puguroad kuja ilala karume polis niaibu hawawalindi raia Tanzania hakuna usalama polisi hakuna binafsisheni polis jamani ni aibu!

    ReplyDelete
  2. Ulinzi shirikishi kati ya POLISI, TANESCO NA HALMASHAURI YA JIJI/ MANISPAA KINONDONI/ILALA kuwasha taa zimulike eneo lote la daraja na barabara jirani na daraja ni muhimu ili tuwafichue hawa majamnazi wakiwa mbali.
    Mdau
    Seaview

    ReplyDelete
  3. Nakubariana na Mdau aliye post hii, daraja la selander si salama kabisa, juzi nimepita pale mida ya saa mbili usiku, nilikuwa sijafunga kioo cha gari, na nilikuwa nimeshika simu, jamaa alikotokea sijui, alikwapua simu na kutokomea kwenye vichaka baharini. Jeshi la Polisi lazima lifanye kitu hapa.

    ReplyDelete
  4. Hata upande wa coco beach si salama kuanzia kwenye mihogo kuelekea coco hao vijana wapo usiku hadi wa manane serikali inabidi iliangalie hili swala

    ReplyDelete
  5. Nashukuru sana kupata nafasi ya kuchangia hapa ningependa sasa hili swala la kigamboni lisiishie hivi hivi waandishi wafuatilie linaendeleaje na wale majambazi na vibaka wanakamatwa na hatua gani zinachukuliwa zidi yao.

    Watu tumekuwa hatuishi kwa raha kigamboni, na cha kushangaza kigamboni kuna vikos vya jeshi, nilitegemea eneo hili liwe salama kwa maana kwamba ni eneo ambalo lina heshima yake kwa kuwa na vikosi vyetu vya ulinzi na usalama wa nchi, inakuaje tena ndo eneo lenye matukio ya kinyama kama hayo.
    Tafadhali Polisi wanatakiwa kufanya kazi yao kwa ufanisi sana hapa kigamboni


    Ni mimi nayeipenda kigamboni

    ReplyDelete
  6. Serikali ichochee ajira,viwanda, masoko mikoani ili vijana waone mataa ya mujini huko Mtwara, Kigoma, Mbeya, Mwanza, Kahama n.k

    ReplyDelete
  7. tatizo polisi wa bongo wapo makini sana kwenye maeneo ambayo watapata kitu kidogo kama kukamata magari mara tuulizwe stika za fire mara triangle bora mradi usemesina uwakatie kitu kidogo maeneo muhimu ya kulinda kwa ajili ya usalama wa rahisi hayawahusu ata kama umeibiwa unaenda kushtaki polisi uwe na kitu kidogo ndio watakushughulikia kwa haraka ,kama umevamiwa ndio kabisa ata ukiripoti polisi waje kukusaidia nyumbani ata kama kituo kipo karibu hawaji pengine uwape pesa yaani inakera, naungana na mdao hapo juu bora wabibasishe polisi

    ReplyDelete



  8. TUTAPIGA KELELE KAMA KAWAIDA LAKINI NO ACTION

    kumbukeni hao beach oys hawana kazi tujue source ya wizi huo kwanza ndo mtawezakurekebisha jamani maisha yamekua magumu siku hizi kazi hakuna mnategemea watakula wapi hao vibaka,,,,,,

    JESHI LA POLISI WENYEWE WEZI NAMBA MOJA UKUMPELEKA KIBAKA UKIRUDI NYUMBANI UNAMKUTA KARUDI KABLA YAKO SASA UNATEGEMEA NINI HAPO

    hakuna la kufanya ndo nchi yetu hii hata upige kelele vipi hakuna atae sikiliza huu tufanye kua uwanja wa mawazo yasiofika kokote pale zaidi ya kumfurahisha michuzi

    ReplyDelete
  9. Cheza Geshi la polisi la Bongo wewe? ah! ogopa askari anachukua rushwa ya shs 2,000/=.

    Cha ajabu hata hawa vijana wezi wanajuana na hawa askari kwani jioni wanachukua 'mshiko' wao na huu ndio ukweli inauma sana sana

    ReplyDelete
  10. Yooote haya mliyosema wadau wenzangu Ni UKWELI Mtupu. Tatizo ni mipango dhaifu iliyopitwa na wakati ya Wenye dhamana na ulinzi wa raia na mali zao MUDA Wote! Aidha Pamekuwa na SHAKA japo haijithibitishi sana Juu ya UWEPO wa maelewano kati ya Waporaji na askari wetu .... Tatizo hili halipo Dar tu - huku mikoani nako lipo sana!! Serikali mtaa/madiwani/wabinge/askari na wananchi tujipange upya Amani Inapotea tartiiiibu tukiona!!

    ReplyDelete
  11. Ukiona watu wanalala mchana sehemu mbali mbali za mji ujue hao wana kazi za usiu. Sehemu nyingi utakuta vijana wamelala, huko baharini sehemu zote vijana wanala, kwenye mabustani ya mnazi mmoja, clock tower wanakaa watu wa ajabu ajabu hata khuwezi kusema nipumzike hapa, usalama hamna. Na nchi hii ukiporwa watu wanakuona na hawafanyi lolote.

    ReplyDelete
  12. UKITAKA KUJUA UKALI WA HUU USALAMA WA RAIA, FANYA MGOMO, ANDAMANA AU FUGA NDEVU HALAFU VAA KANZU NJIWA.

    KUNA MCHANGIAJI ANAPENDEKEZA "SERIKALI ICHOCHEE AJIRA, VIWANDA, MASOKO VIWANDANI", SIKATAI LAKINI NA SUALA LA USALAMA WA RAIA LINABAKI PALEPALE, MBONA KWENYE SUALA LA UJAMBAZI ULIPOZIDI SANA, JWTZ NA USALAMA WA TAIFA WALISHIRIKISHWA? NA MATOKEO YAKE YAKAONEKANA?

    KAZI NDOGO TU, NI KUDHIBITI VILINGE VYAO VYOTE WAKOSE HATA PA KWENDA HAJA KUBWA.

    ReplyDelete
  13. Jamani sio polisi kuchukua sh.2000/= tu, Polisi wanajuana na wezi kwa majina na namba za simu. Ukikwapuliwa laptop ukaenda kutoa taarifa polisi unaulizwa ni eneo gani umeibiwa, ukishawatajia eneo wanakutajia jina la mwizi mkuu wa eneo hilo na kupewa maelekezo ni jinsi gani utampata na unakwenda kutoa pesa ili urudishiwe mali yako. Wakati mwingine unatoa pesa na mali yako bado haurudishiwi.

    Kalungi

    ReplyDelete
  14. naungana na wadau maana nina machungu sana na hawa vibaka wa daraja la selander, niliporwa handbag saa 6 mchana kulikuwa na traffic jam kubwa, jamaa akatokomea nalo kwenye mikoko, namuona hivi, wasamaria wema wakashuka kwenye magari kumkimbiza akapiga mbizi na kutokomea, polisi wako jirani kabisa! hakuna msaada kabisa.

    ReplyDelete
  15. Nadhani ni vizuri kurudisha sungusungu. Kuna mapungufu yake lakini faida zake ni kubwa zaidi kuliko hali ilivyosasa. Sasa Dar imeifikia Nairobi na inampango wa kuipita kulekea kuwa Lagos kwa wizi. Ndugu zangu Dar inajulikana nje ya nchi kama sehemu hisiyo salama. Wageni wanapakwepa siku hizi na kwenda Arusha, Mwanza na Zanzibar. Bila Dictator, Dar haitapona.

    ReplyDelete
  16. Ni katika Jiji la DARISALAMA sio Porini wala Mkoani au nje ya Mji inatokea,

    1-Mwanafunzi wa Chuo mtoto wa Mlala hoi aliyenunua Laptop kwa fedha za Mkopo wa Elimu ya juu, anaibiwa Laptop yake!

    2-Zaidi ya kuibiwa kitu cha gharama ANALAWITIWA au ANABAKWA!

    3-Wanafunzi wanajipanga kudai kuhakikishiwa Usalama wao na mali zao, hao hao Polisi wanaolalamikiwa kuhakikishia Usalama wanawachapwa virungu na mangumi!

    Pana kila sababu Jeshi la Polisi likajirekebisha baada ya kupoteza mwelekeo na Dira!!!

    ReplyDelete
  17. si mnasemaga mkataa kwao mtumwa ha ha haaaa komaeni. chapa mtu risasi hapo salender hawatakaa wapore tena na sirikali itashtuka kiduchu.

    ReplyDelete
  18. polisi tanzania wanalojua ni kupiga mikutano ya wapinzani na kuua raia,na kubambika kesi nithing new of them!yani wanaboa mno
    poleni wahanga na sie

    ReplyDelete
  19. Michuzi tumshukuru sana, angalau anayatoa malalamiko yetu humu na kwa hakika wahusika wanayasoma, japo hawataki kuyafanyia kazi.

    Amani inatoweka kila pembe ya nchi, na WaTz hatuna hakika nani atalifanyia kazi hili, maana sasa hatuelewi kama bora alivyokuwepo Mahita, au Tibaigana, na wengine waliopita - kwani kipindi cha Mh. Mwema kimezidi vituko. Tunawaomba wafanyie kazi kero hizi kote - si Dar tu, mikoani ndio kumeoza. Kulikoni Wizara ya Mambo ya Ndani? Na watu wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kazi yao ni ipi? Mbona twapiga kelele wao wamenyamaza tu! Au na sie tuitwe Nchi ya Kitu kidogo kama majirani zetu!!!!

    ReplyDelete
  20. Nafikiri wakati umefika kuleta wawekezaji wa ardhi ili sehemu zote zipewe wawekezaji. Baadae kila aliyekosa ajira apewe "benefit". Hii itaondosha wizi. Maana wakati wa Mwalimu asiyekuwa na ajira anatakiwa arudi kijijini akalime. Sasa akiwa ardhi itabinafsishwa wasiokuwa na ajira watalipwa "benefit". Umalaya na wizi utoandoka kabisa.

    ReplyDelete
  21. mdau wa tatu anony Wed Jan 16, 03:53:00 pm 2013

    ..umalaya na wizi,

    matendo hayo mawili yanafanywa kwa aina tatu hizi

    i.kwa umasikini na kukosa matumaini
    ii.kwa kutokujifahamu sawasawa
    iii.kama maradhi au hulka binafsi (hapa unakuta mtu anafanya wizi au umalaya ilihali akiwa anatokea kwenye familia isiyo na shida zozote kiuchumi au uwezo)

    katika hayo mawili wapo wayafanyao kama maradhi ya hulka au tabia binafsi hivyo ikiwa ni hapo hayana dawa wala suluhisho la kudumu kama (iii) hiyo.


    ReplyDelete
  22. Na sisi wananchi tumelala!kwanini tusitoke tukaandamana tena?tukatowa nguvu kwa wanafunzi tunalichukulia rahisi swala la kulawitiwa jamani hawa vijana wataishi vipi katika maisha yao?kwakweli hiki nikitu kibaya sana ingekuwa ni ulaya hilo jeshi la polis lingejieleza na wao ndio wenye majukumu ya kuwalipa hao vijana walio lawitiwa!nimbaya sana watanzania hatupendani na pia serikali haipendi raia wake haya maswala sio madogo!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...