Na Maggid Mjengwa,
Ndugu zangu,
Kwenye jamii yetu kuna mjadala wa gesi. Kila ninapoufuatilia mjadala huu naiona hulka ya baadhi ya viongozi wetu inavyodhihiri; kuwa wanachanganya siasa na gesi. Kuna hatari ninayoiona ya nchi kulipuka. Ni wanasiasa walioelekeza mjadala wa gesi ubebe sura ya kimaeneo na kikabila. Na nahofia si muda mrefu tusasikia dini nayo ikichanganywa na gesi. Hapa kuna tatizo kubwa. Kinachokosekana ni ufahamu wa jambo zima kuhusu rasilimali zetu za nchi na nani wa kumnufaisha.
Tumefika mahali Watanzania tumekuwa kama wale watu wanaogombania bakuli za supu kwa ng’ombe ambaye hajachinjwa, na pengine hajatolewa hata zizini. Fikiri kama ng’ombe atakata kamba au kutoroka zizini.
Tumefika mahali baadhi ya wanasiasa kwa kauli zao, wanawafanya Watanzania waamini kuwa neema ya gesi kwao itapatikana kesho au kesho kutwa. Si kweli. Kimsingi manufaa ya gesi hii, kama itasimamiwa vema, ni kwa watoto na wajukuu zetu. Hii si gesi yetu, ni ya vizazi vijavyo. Ujinga ni kutaka kuitumia gesi ya vizazi vijavyo kama karata kwenye siasa zetu za sasa za reja reja- retail politics. Ndio hii hatari ninayoisema ya kuchanganya gesi na siasa.
Ni dhahiri, kuwa muda wetu wa kuishi humu duniani ni mfupi sana. Tofauti na wanyama, binadamu katika maisha yetu ya duniani, tuna kawaida ya kufikiria hiba ya kuacha nyuma yetu, kwa familia zetu na kwa jamii tunayoishi.
Fikiri mtoto uliyemzaa akikuuliza; “ Mama/ Baba, ukiondoka hapa duniani ungependa tukukumbuke kwa yepi?
Hilo ni swali gumu kwa yeyote anayeulizwa. Majibu ya swali hili yanatusaidia kuelewa umakini wa anayejibu. Swali hili linahusu hiba ya mtu anayoiacha nyuma yake. Hiba ambayo angependa akumbukwe kwa kuhusishwa nayo, ni urithi. Wazungu wanaita “Legacy”.
Maharage na mahindi yakipikwa pamoja unapata makande. Nyama na mchele unapata pilau. Sijui ukichanganya vyaote, yaani mahindi, maharage, nyama na mchele unapata kitu gani?
ReplyDeleteKinachotokea sasa ni mfano wa watoto marafiki wanaocheza na kula pamoja kwa miaka tele. kati ya hao watoto mmoja kwao wana ahueni kimaisha lakini wakati wote hukaribishana na kula pamoja kilichopo. sasa aliyekuwa kwao uwezo umepungua mzazi kapata uwezo na mtoto wake kwa habari hizo kaukataa urafiki na anasema kila mtu sasa akale kwao!!!!!
ReplyDeleteTanzania hii kwa miaka zaidi ya hamsini imeendeshwa kwa uchumi wa mazao machache kama kahawa, pamba, n.k.sasa gasi inapatika umeenza mchezo wa chako chetu , changu changu!!. Na watu washashabilia macho makavu?
Mdau Anonymous wa Sun Jan 13, 11:38:00 pm 2013
ReplyDeleteJIBU:
Mchanganyiko wa Mahindi kwa Maharage na Mchele kwa Nyama vyote vinne (4) kwa pamoja unapata MCHANYATO ama GITHERI (Kwa Watani zetu wa jadi KENYA)
Ni aina ya lishe ambayo yataka moyo kwa mlaji, kwa wale wenye mchango mwepesi waweza kutapika!
...Na ndicho wanachotarajia kuvuna wanaochanganya GESI na SIASA ZA KIBONGO!!!
Ndg. Mjengwa,
ReplyDeleteUmetoa Makala ya maana sana!
Lingine la Muhimu ni kuwa tuachie maamuzi ya Kitaalamu yafanye kazi kwa kuwa hatukuwa na Uchumi wa Gas na Mafuta hapo kabla, tulizowea Uchumi wetu wa Kilimo cha mazao ya chakula na Uchuuzi wa Mazao ya Wakulima Sokoni.
Hivyo ni sawa na Kiwanda cha Bidhaa za Kisasa na Mitambo ya Kisasa akakabidhiwa Muua Genge!
Pana mambo mengi ya muhimu kuundwa kabla ya mafao hayajapatikana kama Makala inavyosema.
La muhimu hao wana Siasa wangefanya la maana kama wangechangia Sera za Maana ili kufikia lengo hilo kwa uharaka zaidi na uhakika kuliko kuwatumia wananchi ili kupata Umaarufu wa Kisiasa.
Wananchi Lindi na Mtwara mngezingatia kwanza Kilimo cha Korosho na Uvuvi wa samaki kabla hamjarukia kwenye mavuno ya Gesi!
ReplyDeleteAma mngewashauri wana Siasa mnaoshirikiana nao muanzie kwenye Sekta za Uhcumi wa awali (KILIMO CHA KOROSHO NA UVUVI WA SAMAKI) kabla hamjarukia Uchumi wa Kisasa wa gesi na mafuta!
Ndugu Wadau wa Blog na hasa ndugu Mjengwa, Naomba niwasalimie, kwanza salaam!! Pia naomba nichukue nafasi hii kujibu hoja iliyowekwa mbele !!mimi naona hatari kubwa ipo katika vyombo vyetu vya habari na waandishi mnavyochangia kuupotosha umma !! Ukisoma kichwa cha habari yako kinasema « Gesi ; tunagombania Bakuli za Supu, Ng’ombe hajachinjwa !! » Kwanza kabisa inaonyesha ni jinsi gani mwanablog anaupotosha umma, naomba nianze kumuelimisha kuhusu uandishi wako na sakata zima la gesi kwa kiasi tu:-
ReplyDelete1. Nikianza na picha aliyoiweka katika habari hii (Sina uhakika kama inahusika na gesi Mtwara) picha halisi ya eneo husika zipo hata kwa kugoogle tu mkuu au kuomba wadau Mtwara wakapiga picha na kukutumia, kuna picha za utafiti, Mitambo midogo ya kufua gesi, picha za survey plan ya bomba litapita wapi, picha za ofisini, Ramani mbalimbali na vionjo vyingine vinavyoonyesha uhalisia wa habari yako na mazingira halisi, ili hata msomaji aelewe kweli huyu ngombe hajachinjwa!!!
2. Mwanablog amezungumzia kuwa tunagombania Bakuli za Supu, Ng’ombe hajachinjwa (kwanza naomba afute kauli yake na kuwaomba radhi wasomaji maana huu ndo tunaouita uhuni au siasa za rejareja alizozisema yeye mwenyewe). Kwa taarifa yako, kihistoria gesi iligundulika Mtwara (eneo la Msimbati/Mnazibay) miaka ya 1982 baada ya kukamilika kwa tafiti. Kuanzia mwishoni mwa mwaka 2004 gesi ya Mnazibay ilianza kuzalishwa na kampuni ya Artumas ambayo baadae iliuza hisa zake na kununuliwa na kampuni ya Wentworth Resource,
Sasa gesi inazalishwa Mtwara na inatumika kufua umeme kama ilivyo kwa Songosongo-Ubungo, leo unaposema tunagombania bakuli za supu, ngo’mbe hajachinjwa, sijui unamzungumzia ng’ombe mtu au unajifurahisha kuandika!! Angekuwa hajachijnwa hivi serikali ingeingia mkataba haraka haraka wa kujenga mtambo wa kufua na kusukuma gesi na pia kujenga bomba la gesi kutoka mtwara na kuileta Dar!!
3. Wananch wa mtwara wanasikiliza ahadi za serikali, sasa nani anatia siasa za jareja, nadhani wewe ndo wa kwanza kulitekeleza hilo kwa habari ulioiandika hapa ambayo haileweki kuwa ulikuwa unaandika stori za mtaani/vijiweni au hadithi za kusadikika !!!
4. Wananchi wa Mtwara wanataka ajira na sio vibarua
5. Nina mengi ya kuwaeleza na kwa takwimu kabisa (leo sijatumia takwimu wala vielezi vya wenye dhamana na wawekezaji) lakini muda hautoshi,
6. Mwisho ukikakaa katika eneo linalolimwa michaichai au mauridi lazima michaichai/mauaridi yaonekane na lazima panukie michaichai au mauaridi na wala sio panukie mializeti/mikaratus au paonekane siasa tu hakuna vitendo !!!!