Mwenyekiti wa asasi  ya siasa ya Ulinzi na Usalama ya nchi za Jumuiya ya maendeleo ya nchi kusini mwa Afrika (SADC) Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine ambao ni wajumbe wa asasi hiyo wakati wa mkutano wa siku moja uliofanyika ikulu jijini Dar es Salaam leo.Wapili kushoto ni Rais Jacob Zuma wa Afrika ya Kusini,Rais Armando Emilio Guebuza wa Msumbiji(Watatu kushoto),Rais Hifikepunye Pohamba wa Namibia(kulia) na wa kwanza kushoto ni Katibu mkuu wa SADC Dr.Tomaza Salomao. Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Nawapongeza sana Viongozi wetu wa Afrika!Nakupongeza sana Rais wetu,Kikwete,kwa hili,wala sitafuni maneno!Nawapongeza kwa dhati kabisa kutoka moyoni mwangu!Hii inanikumbusha enzi za Uongozi wa Mwalimu Nyerere,wakati huo harakati za ukombozi mwa kusinimwa Afrika ulikuwa umepamba moto,miaka ya Sabini!Ilikuwa ni kawaida kabisa Viongozi kutoka nchi hizo kukutana Dar es salaam,wengi wao wakiwa bado "Mafichoni!".Polepole,idadi ikazidi kuongezeka ya viongozi wa nchi huru za kusini mwa Afrika.Nguvu ya Pamoja ikazidi kushika kasi!Hatimaye,nchi zote kusini mwa Afrika zikajikomboa.Na leo hii,kwa kweli "inatupa fahari watanzania,pamoja na umaskini wetu",kuwaona Viongozi hao,wakikutana pamoja katika mazingira ya Udugu kabisa,ili,kuzungumzia matatizo yanayo wakabili Majirani zao,Congo DRC,Madagascar,Afrika ya Kati,na kwengineko!Ni fahari kubwa kwetu sisi Watanzania!Keep it Up!Viva Mzee Nelson Mandela,Babu yetu,Babu wa Afrika Huru!The Spirits of Julius Kambarage Nyerere shall live on!Never say Die!....(to.....y)

    ReplyDelete
  2. Hawa ndiyo viongozi dume halisi wa Afrika.Siyo viongozi wanna be Rais wano tumwa kugawanya nchi na kuleta confusion wakati wanashindwa kuongoza nchi zao.Hongera na mapenzi makumbwa kwa viongozi.Kila kheri.Mungu Ibarike Afrika pamoja na viongozi wa ukweli.Learn something bwana wazir wa nchi za nje.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...