Baadhi ya askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania wakimshusha mwenzao baada ya kujigonga kwenye mti na kujeruhiwa vibaya sana kwa kupasuka kichwa wakati akiwa kwenye Lori lenye namba za usajili 5514 JW 07 aina ya IVECO kandokando ya barabara ya Samora jirani na Idara ya Habari (Maelezo) jijini Dar es Salaam jioni hii. (Picha na Habari Mseto Blog)
Baadhi ya wasamalia wema wakimpeleka hospitali majeruhi huyo.
Majeruhi akiingizwa katika Bajaji tayari kwa ajili ya kupelekwa hospitali.
Hii ndio Barabara ya Samora ilipotokea ajali hiyo.
Hapa ndipo alipojigonga majeruhi na kupasuka kichwa.
Ndugu mwandishi tafadhali sana,tunaomba uwe unafahamu unachokiandika maana habari yenyewe ukiisoma hata haieleweki hadi urudie mara mbilimbili ndio uelewe.Ulipaswa kuweka kwa ufupi tu habari yako ili iweze kuleta maantiki,maneno mengi lakini yanajiumauma tu
ReplyDeleteAsante
Haya sasa mjadala wa ni gari lipi linapaswa kubeba majeruhi ushahidi ni huu - yaani katikati ya jiji hakuna huduma za dharura za papo kwa papo na badala yake majeruhi anabebwa na bajaji kwenda kupata huduma ya kwanza hospitalini!! Bongoland ni zaidi ya uijuavyo!!!
ReplyDeletePole sana majeruhi. Swali langu KUBWA ni "Je, hawa wanajeshi sheria za nchi hii haziwahusu?" Maana inaonekana wazi kuwa lori lilikuwa wrong direction, hiyo njia haitoki kwenda kwenye askari, imekuwaje wao wanaelekea huko. Sheria ifuate mkondo wake, msumeni unakata huku na huku
ReplyDeleteJapo ni ajali imetokea, bado ni fundisho pia kwa chombo husika cha Dola. Kuwa ajali hiyo kwa huyo askari wa jehi ingeweza kuzuilika kama endapo chombo husika(Police- Kitengo cha Traffic) wangefanya kazi yao.Ukweli ni kwamba Traffic waliona uzembe uliofanyika kwenye upakiaji wa mizigo kwenye hilo Lorry, lakini kwasababu ni Lorry la Kijeshi,na pengine aliyekuwa na mizigo ndani ya lorry ni mwanajeshi, basi Traffic wakaamua kufumbia macho Road Traffic Offence,which is Overloading. Dereva wa hilo lorry anatakiwa kuwajibika- kwa kosa la ku overload, na pia Traffic officer aliyyekuwa on duty siku hio na saa hizo katika maeneo hayo anatakiwa awajibishwe, maana ni wazi kabisa alizembea na kuacha kufuata taratibu zake za kazi. Period.
ReplyDeleteTraffic asilaumiwe coz njia hiyo kwa mida hiyo hakuwepo hata mmoja na isitoshe barabara inajulikana vizuri kuwa ni one way trafic. Hapa uzembe uliofanyika pia ni wa majeruhi mwenyewe kana kwamba alikuwa hafahamu au haoni miti iliyokuwepo barabarani. Kumbukeni kukaa hata nyuma ya pickup hapo nyuma ilishapigwa marufuku kutokana na abiria wengi kuanguka na kusababisha ajali. Pia inaonyesh dereva alikuwa kasi hadi kusababisha majeruhi kupasuka kichwa. Poleni sana ndugu na jamaa wa majeruhi
ReplyDeleteDespite the high risk of infection from the blood,the good samaritans would not care less, the held the chap and actually perform a very good first activity of applying pressure on the bleeding wound, and then came bajaji for the rescue, well to do people gave ambulances to an already well off Hospital, bongoland arosto.
ReplyDeletepole majeruhi but ili lile fundisho siku zote hawa wanajeshi wanajiona wako above the law hata wakivunja sheria ni sawa tu kwao.Nanyi trafic sio kusimamisha maloli ya mizigo na mkaa tu ili mpate kitu kidogo, mkiona gari limebeba mizigo na watu wanasimama juuyaani wananinginia inabidi mlisimamishe mchukue hatua sio kubebana kisa wanajeshi mkome
ReplyDeleteWatanzania tunapashwa kubadilika sasa. Wekeni first AID kits kwenye magari yenu. Kesho hao jamaa wawili waliombeba na kutoa msaada wa kwanza kwa mwenzao wakipima na kukutwa na UKIMWI wanaanza kugombana na wake zao bure wakidhani ni ngono zembe ndio iliyoleta UKIMWI kumbe ni damu ya mwanajeshi mwenzao! Sina maana kama huyo mwanajeshi ana UKIMWI ila walichofanya hao jamaa ni ujasiri mkubwa ila kama mwenzao alikuwa na maambukizi hapo kuna chance kubwa ya kuwaambukiza na wao. Tuchukue tahadhari na tuyapende na kuyajali maisha yetu.Nawashauri wakapime Afya zao na kuanza PEP (Post Exposure Prophylaxis) haraka sana.
ReplyDeleteCha ajabu wanajeshi wenzao wamekaa ndani ya lori wanakenua tu! Wananchi ndo wako mstari wa mbele... Aiseee....
ReplyDeleteImekuwaje Askari Jeshi wasimsimamie Mwenzao baada ya kupata madhara ya ajali?
ReplyDeleteKwa nini wasitumie gari lao la Jeshi wenyewe kumpeleka majeruhi Askari mwenzao Hospitali kwa Bajaji huku wakiwa wako mbele ni raia?