Hosteli ya wanafunzi wa chuo cha Utumishi kilichoko manispaa ya
Mtwara/Mikindani yakoswa koswa kuchomwa moto hii leo kwa kile
kinachodhaniwa kuwa na uhusiano na Hawa Ghasia pamoja na kituo kidogo
cha Polisi Cha Shangani mkoani Mtwara.
Vurugu hizo zilizoanza jana,leo zimehamia wilayani Masasi mkoani
Mtwara ambapo Inasemekana Askari mmoja wa Upelelezi wa jeshi la Polisi
Ameuawa baada ya kujiingiza katika kundi na kubainika akiwapiga picha
ambapo pia alikutwa na bastola 2 huku Nyumba ya Mbunge wa Masasi(Mama
Kasembe),Vifaa vya Mahakama ya mwanzo pamoja na magari ya Halmashauri
nayo yateketezwa kwa Moto mchana wa leo katika vurugu za waandamanaji
zilizoanzishwa na watu wa Bodaboda.
POLISI walianza kutuliza ghasia hizo na baadae wakazidiwa
na kulazimika kupiga mabomu ya machozi na risasi za moto.
Taarifa ambazo hazijathibitishwa na Mamlaka yeyote hadi hivi sasa
kufuatia simu za mkono za viongozi wa polisi kutopokelewa ni
kwamba wananchi wanaendelea kufanya uharibifu mkubwa katika mji huo ambapo
Polisi wamezidiwa na wamejifungia kituoni wanarusha mabomu yao tokea
huko walikojificha maana nje hakutamaniki.
Na wameshateketeza nyumba
ya mama Kassembe,Mbunge wa Masasi
Kikao cha dharura cha kamati ya ulinzi na usalama kinaendelea kwa
kuwashirikisha maafisa wa polisi na maafisa usalama waliotoka Dar es
Salaam kuongezea nguvu. Maaskari na makachero wamewasili Mtwara leo
asubuhi na helkopta kuongezea nguvu.
Maandamano hayo ya Vurugu yalioongozwa na Madereva wa boda boda.
Risasi za moto na mabomu ya machozi yanapigwa kutawanya watu na tayari
nyumba moja imechomwa moto na baadhi ya magari huku Vijana wakizidi
kusonga mbele
Tanzania nchi yetu inakwenda au kupelekwa wapi? Nani anayo tafsiri sahihi juu ya haya yanayotokea? Mapambano ya wananchi na vyombo vya dola siyo dalili nzuri kabisa. Na hasa inapoonekana kuna kila dalalili ya vyombo vya dola kushindwa kuwadhibiti wananchi kwa njia zozote iwe za amani au nguvu. Rejea machafuko ya Dumila, Zanzibar na sasa Mtwara. Kweli Vingozi tulio nao wanafanya kazi kwa uwezo wao wote? Je vyombo vya usalama vipo makini vya kutosha kujua na kukinga madhara yanayoweza kuipata nchi yetu? Kama sivyo, tunajiandaa kukimbilia wapi? Ni Msumbiji, Kongo, Kenya, Zaire, Zambia au Malawi? Hii ndiyo demokrasia na malipo ya uhuru na haki za binadamu ambazo tumekuwa tukipigania kwa miaka mingi? Wanasiasa na wataalamu katika masuala ya Uchumi, Sayansi, Dini na Sheria, mnajambo lolote la maana kuiambia jamii ya watanzania kuhusiana na haya yote yanayo jitokeza kwa kasi? Yapo mambo mengi ambayo hayajapatiwa ufumbuzi, kama vile mabadiliko ya katiba, Gesi Mtwara, Muungano Zanzibar, Vurugu za kidini, Janga la njaa ambalo linakabili mikoa mingi na mabadiliko ya hali ya hewa. Tunaomba wale tuliowakabidhi dhamana ya kutuongoza waonyeshe kwa vitendo ile nia yao njema waliyoahidi katika kampeni au wakati wanaomba nafasi hizo.
ReplyDeleteHii ndo Tanzania Tunayoitaka?
ReplyDeleteNi dhahiri kwamba Kunakitu hakiendi sawa sehemu fulan (something is wrong some where) sidhan kama kweli tukiwa katika karne ya sayansi na technolojia hii ndo tanzania ya ndoto zetu. Najiuliza maswali mengi
Je ni kwamba hawa waandamanaji kweli hawajui wanachokihitaji au kama wanajua hawajui jinsi gani ya kukidai
Je ni serikali haijui mahitaji ya wanachi wake
Je ni Mfumo wa Intelijensia (intelligence system) ya nchi haufanyi kazi yake vizuri au mtandao wake ni dhaifu kuweza kujua haya yote kabla hayajafikia hapa
Je ni uelewa mdogo wa wanacnhi kuweza kupambanua mambo vizuri
Je ni uwezo mdogo wa washauri wa serikali hivyo kusababisha serikali kufanya maamuzi mapungufu mengi
Je ni serikali inapuuza hoja za msingi au ni wananchi wanapuuza maamuzi ya msingi ya serikali?
Jaman nisaidien hii list ya maswali inaweza kufika mtwara na sina majibu Tatizo nini
Du kwa hiyo ukiwa na nyumba ya vioo tuu kosa! Jamani kila mtu kwa nafasi yake ajiangalie kakosea wapi turekebishe mapema hii hali sio nzuri kabisaaaaa. Mdharau mwiba........
ReplyDeleteje mikwaju hamna huko au visiwani tu?
ReplyDeleteInasikitisha kuoa nchi yetu ilipofikia, watanzania tuliakua watu wa kuheshimu nchi yetu na mamlaka , lakini viongozi wetu ndo wamefanikisha kuzalisha tunayo yaona sasa. Imebakia waanzer kuchoma na watoto wao ndio hapo viongozi wetu watapojifuza kuwa an adabu
ReplyDeleteKiukweli Serikali inabidi itafakari hii hali kwa kina zaidi na kutafuta suluhu ya MUDA MREFU na sio za muda mfupi. Kiukweli wananchi wamechoshwa na maswala yote yanayoendelea katika vyombo vya Serikali ikiwemo KUKITHIRI kwa RUSHWA.
ReplyDeleteNadhani Serikali ingepitia suala la sheria kuhusu RUSHWA na UFUJSJI wa mali ya UMMA na kuongeza ADHABU yake kwakuwa haya ndio mambo yanayoweza kuharibu AMANI ya Nchi hii
Siwezi kuamini, serikali imekaa kimya mpaka sasa hivi wakati watu wanafanya watakalo. Mimi najiuliza, kuchoma moto magari ya halmashauri, nyumba za watu na hata ambulance kinamuumiza nani kama sio mwananchi mwenyewe? Huu ndio upeo wa kufikiri wa watu wa kusini. Na ndio maana mikoa hii mpaka leo haijaendelea. Wawekezaji wakiondoka ndio wataona joto ya jiwe! Upuuzi mtupu! Ankal usiiminye hii!
ReplyDeleteTunaelekea wapi sasa?.?Tunachezea amani yetu eh?
ReplyDeleteDavid V
Rais Kikwete, vitu kama hivi vinatokea kila kona ya nchi ukivifumbia macho ndo pale unasikia kuna vita vya wenyewe kwa wenyewe. Sidhani kama ni vizuri umekaa kimya namana hiyo na mambo yanaendelea kuwa mabaya ni sawa, haya siyo mambo ya kuwaachia FFU au Mkuu wa mkoa hapana yameshawazidi tayari ninavyoona mimi, FFU hapa wanaongeza chuki tu ninavyoona mimi hamna lolote, tunahitaji mtu mzima kama wewe usimame kukemea mwendo huu.
ReplyDeleteMimi naitwa Xavery komba niko Mbinga.
kumbe inauma kweli sisi Wazanzibat mikituonea munasema wabaya Watu wameshachoka na c.c.m.
ReplyDeleteAnkal ukiitia hii comment kwenye bin sawa lakini huo ndio ukweli.
wamachinga wanajaziba vile vile kufukuzwa mtaa wa congo na dar kwa jumla biashara zao kuchukuliwa na mitaji yao ya kuuza korosho za msim lazima walipize kisasi sasa..kweli wamachinga wameamua sasa inabidi serikali iangalie kustopisha suala hilo zima kutafuta ufumbuzi...
ReplyDeletendugu zangu hii sio habari ya ccm au siasa! Tuache kutafuta majibi mepesi kwa maswali magumu. Mfumo uko shakani na vyema serikali NA WANANCHI wakajiuliza na kujiangalia upya. Nina wingu huko mbele: Ivory coast ilikuwa na amani kuliko hata Tz ya miaka ya nyuma lakini walianza polepole HIVIHIVI - haikuwachukua muda na hadi leo miaka zaidi ya 10 wanachinjana!
ReplyDeleteSerikali iko wapi???????
ReplyDeleteKama watu wanapoteza maisha na mali kuharibiwa hii kama siyo vita ni nini?
Serikali kuu na vyombo vya usalama lazima vichukue hatua mapema. Tusiudharau huu mwiba!
No Risk, No Reward.... sometimes fujo zinatakiwa ili watu wajue kuwa kuna-usiriaz wa maisha na maendeleo.
ReplyDeletedu jamani viongozi wa dini mko wapi pigeni goti kuombea amani Tanzania ndio amani inatoweka hivyo kama mkoa kama wa mtwara ambao wananchi wake wanaonekana wanaupeo mdogo wanaweza kufanya uharibifu mkubwa hivi je mikoa ambayo inaonekana watu wanauelewa mkubwa nao wakianza kupinga kitu na kuanzisha fujo si itakuwa balaa
ReplyDelete