Habari Michuzi Team,
Naomba muipost hiyo picha hii ili wahusika waweze kufyeka hivyo vichaka. Hili ni eneo la njia panda ya chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM) karibu na daraja la Ubungo barabara ya Sam Nujoma.
Unapotoka Mlimani City ukifika njia panda hiyo kwenye mataa karibu na daraja, unapokata kwenda UDSM huwezi kuona vizuri magari yatokayo Ubungo mataa na hivyo ni rahisi kutokea ajali na hasa ukizingatia kuwa magari mengi huja kwa kasi eneo hilo.
Naomba wahusika mlifanyie kazi swala hili.
Asante sana mkuu kwa kukiona hicho kichaka kamkitu hatari sana kwa usalama.Hiyo watu wa usalama na Afya(safety and health) wanaita HAZARD(Hatarisho??).Yaani umegundua HAZARD.Sehemu zingine za kazi(zinazojali usalama wa wafanyakazi wake) ukigundua kitu kama hiki unaweza kupata zawadi.
ReplyDeleteDavid V
Eh, usichokijua nini wewe.? Kila siku tunalalamika uharibifu wa misitu wewe unalalamika!
ReplyDeleteKutokana na mvua zilizonyesha kwa mfurulizo, mahani yameweza kuota ghafla kuliko kawaida. Tunaahidi kusafisha hayo maeneo ndani ya siku mbili.
ReplyDeleteUmeongea vizuri, halafu unachanganya na maneno ya utani au? barabara na road kunatofauti gani? Tunapoelimishana ama kukumbushana kuwe na lugha inayoeleweka.
ReplyDelete